Pre GE2025 Wananchi wa Kilimanjaro wachangishana kurekebisha barabara mbovu yenye urefu wa kilomita 72

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Safi kabisaa. Hiyo ndio dhana halisi za siasa ya ujamaa na kujitegemea. Naimba mfano huu uchukuliwe kwa watanzania wote, wajue maendeleo watajiletea wenyewee.
Wananchi wakiwajibika kujiletea maendeleo wenyewe kwa mtindo huu, jukumu la serikali kitakuwa lipi na suala la kodi na mapato mengine ya taifa (misaada, mikopo) yatashughulikiwaje?
 

Watu wanahangaika, barabara hazipitiki, mwenzetu anazurura na wasanii nje ya nchi akiwalipa posho ya sawa na sh. 2.7m kwa siku, huku wakiwa wamelipia gharama zote.

Nitashangaa sana kama hao wanaohangaika barabara zao, atapatikana hata mmoja wa kumpa kura!!
 

Hiyo inathibitisha, Serikali haijishughulishi na adha zinazowakumba wananchi.
 
Safi kabisaa. Hiyo ndio dhana halisi za siasa ya ujamaa na kujitegemea. Naimba mfano huu uchukuliwe kwa watanzania wote, wajue maendeleo watajiletea wenyewee.
Basi hata kodi wasamehewe, ili hiyo pesa ambayo wangetoa kodi, wawe wanaamua waitumie kwa kazi gani kwenye maeneo yao.
 
Ni ijungaa bado nasisitiza kodi zunatumika wapi?; haya yakiendelea kuna siku Raia wataambiwa wachangishane wawalipe watumishi wa umma mishahara.Huu ni ujinga kodi zijenge Barabara haiwezekani.

Mbona tayari yameanza. Sekondari nyingi, hasa za vijijini, wazazi wanachangishana kuwalipa posho walimu wa kujitolea kwa sababu walimu walioajiriwa ni pungufu ya mahitaji.
 
Uongo wanini? Nimekwambia mmechelewa sana, Mwanza wameanza zamani sana, tena kiwango cha mawe, unabisha hilo nikuwekee ushahidi?
Ndio maana nimekwambia huo ni uongo, kama ni kweli tuambie ni kijiji gani huko Mwanza wananchi waliojichanga kutengeneza barabara za mawe kijiji kizima?

Wewe unajua barabara za urefu wa km 72? Wape maua yao tu hao wachaga na wakristo wa huko Kilimanjaro.
 
Kwanza wagomee kulipa kodi kwa maana haiwasaidii zaidi ya kugharamia anasa za watawala. Baada ya hapo ndiyo walistahili kuanza kuchangishana.
Lini wagomee kulipa kodi na lini waanze kuchangishana?
Wagomee kivipi?
 
Wananchi wakiwajibika kujiletea maendeleo wenyewe kwa mtindo huu, jukumu la serikali kitakuwa lipi na suala la kodi na mapato mengine ya taifa (misaada, mikopo) yatashughulikiwaje?
Jukumu la serikali kwa wananchi ni maeneo mengi saana, mfano, amani, ajira, kupandisha madaraja watumishi, kujenga vituo vya afya na kusambaza huduma mbalimbali katika jamiii, kama vile umeme shule n.k, n.k
 
Basi hata kodi wasamehewe, ili hiyo pesa ambayo wangetoa kodi, wawe wanaamua waitumie kwa kazi gani kwenye maeneo yao.
Na waganga, wauguzi, walimu, wanajeshi n.k n.k watalipwa na nini sasa ndugu yanguu??
 
..asilimia 60% ya mkoa wa Kilimanjaro ni wilaya za Same na Mwanga. Je, hali ya maeneo hayo kimiundombinu ikoje?
Barabara nyingi za Same na Mwanga za Vijijini ni za vumbi, zilianza kuchimbwa kwa kuchoronga mlima na miamba na wananchi wenyewe (kwa zana duni za mikono) kabla ya Uhuru na bara bara hizo zinakwenda milimani ndani ndani, zinapitika mwaka mzima na zipo mpaka leo hii. Hii ni asili yao kupitia utamaduni wao maarufu wa Msalagambo. Ndio utamaduni uliozalisha maendeleo ya kijamii ya kudumu. Hii inapaswa kupongezwa na kuigwa.

Kwa Mwanga, upande wa Usangi na Ugweno (maeneo ya vijiji vya asili vya wapare) wana barabara za lami iliyochipuka katika barabara kuu ya Dar-Moshi, barabara hizo zinafika huko milimani, juu kabisa, ndani ndani kabisa. Hii ni barabara ya upendeleo tu kwa heshima ya wazee wao kina Kisumo, Mgaya, Msuya, Asha-Rose Migiro, Maghembe na utitiri wa Mabregadia wastaafu wa jeshi ambao wameporomosha majumba mazuri na wanaishi huko na kuzikwa huko.

Maeneo ya mjini katika wilaya za Mwanga na Same kiujumla yana lami, ni sawa tu na makao makuu ya wilaya nyingi hapa Tanzania.
 
Wananchi wakiwajibika kujiletea maendeleo wenyewe kwa mtindo huu, jukumu la serikali kitakuwa lipi na suala la kodi na mapato mengine ya taifa (misaada, mikopo) yatashughulikiwaje?
Nakwambia hao jamaa wa huko Kilimanjaro ni akili kubwa sana, ungewaelewa usiandike hayo.
Kukupa mwanga tu, issue iko hivi. Serikali ni watu, na ukitaka kuwawin wasome walivyo na wanavyofanya mambo yao. Hao wachaga baada ya kujichangisha pesa walienda TARURA, na huko TARURA kwa aibu ikabidi waunge mkono juhudi zao! Wewe endelea kusubiri serikali ikulteee maendeleo tu.
 
..Watz wengi wameaminishwa kwamba Kilimanjaro "imependelewa" kwa miundombinu ya kila aina. Hata ukisoma mijadala mbalimbali hapa JF utakutana na hoja za namna hiyo.
Huyu aliyesambaza hiyo 'sumu' amefanikiwa sana kwasababu inaonekana ni kweli

Jambo moja, Wananchi wa Kilimanjaro wamejitolea sana kwa maendeleo yao. Kuna barabara zimejengwa miaka 1950 kurudi nyuma kwa njia za kujitolea tena kwenye milima na miamba

Ukisoma habari hiyo, Wananchi wanasema '' Uharibifu wa barabara umezuia shughuli zao'' kwa maana kwamba ndizi na mazao mengine yanaoza. Ni rahisi kuchanga kidogo upate mahali pa kupita mengine yatafuata.
Habari inasema '' hata waliokuja Pasaka walipata tatizo'' na ndio faida ya watu kurudi makwao kila nyakati

Swali la kujiuliza, Mbunge yupo wapi? Mwaka 2025 utasikia '' nichagueni niwaletee maendeleo''
Mbunge alitakiwa awepo kusaidia 'coordination' ya shughuli hasa kwa upande wa serikali.

Gharama za KM 72 ni kiasi gani ili tulinganishe na V8 kisha tujiulize kodi tunalipa za nini?

Swali la mwisho, haya yanatokea miaka 60 baada ya Uhuru! tutaendelea hadi lini? Tunahitaji mbadala?
 
Kuna umuhimu wa kuwa na serikali za majimbo tu. Kila mikoa ijitegemee kiuchumi/kikodi sio wote wanalipa kodi ila walaji wawe wabunge wa daslamu tu na maV8 mapya.
 

..wilaya ya Mwanga inaweza kuwa ndogo kuliko zote Kilimanjaro.
 
kungekua hakuna kulipa kodi hizo za kodi watu waendeleze mitaa yao kuna sehemu bongo kungekua kama new York
 
Hawalipi Kodi? Yaani Kodu walipe zineende kununua wapinzani, kulipa Bongo Muvi kule Korea then Raia wachangishane kijenga Barabara. Wachaga wamenza ufala
Serikali ipo, Mbunge yupo TARURA ipo hizo pesa wanapangiwa zinaenda wapi?
Hata mbunge ana Mil 500 kila mwaka za maendeleo.
!!
Hongereni sana wanakijiji mjijue ni wapi pakuelekeza kura zenu uchaguzi ujao!!
 
Excellent!
Wrong!
Wilaya ya Mwanga ipo milimani ' Ugweno na Usangi' ambako kuna population kubwa sana na shughuli nyingi sana. Hospitali ya Wilaya ipo Usangi. Shule nyingi za sekondari zipo milimani. Kumbuka kuna kilimo cha ndizi, kahawa, Iliki n.k. Kwa ufupi pale Mwanga unapopaona ni kwasababu ya ''convinience'
Lami kwenda Ugweno na Usangi si upendeleo ni kwasababu ya shughuli za kiuchumi za Wilaya.
Maeneo ya mjini katika wilaya za Mwanga na Same kiujumla yana lami, ni sawa tu na makao makuu ya wilaya nyingi hapa Tanzania.
Wilaya ya Mwanga pale barabarani ni Lami ya barabara kuu hakuna kitu kingine.
Nimekueleza kwamba Wilaya imewekwa pale Mwanga ili kupunguza umbali na watu wa Bondeni kuanzia Nyumba ya Mungu, kuja Lembeni hadi Same na watu kutoka Lake Jipe hadi Njia panda.

Wilaya ilipaswa kuwa katika maungano ya Usangi na Ugweno lakini pia walizingatia maeneo ya Bondeni ikaamuliwa ijengwe pale Barabara kuu ya Moshi-Arusha

Kuhusu Same, ni Wilaya iliyodumaa kwasababu tangu Mkoloni imekuwa Wilaya na Boma.
Harakati za kupinga kodi '' Kodi ya Mbiru' dhidi ya Wajerumani ilifanyika Boma Same wakati huo ikiwa pamoja na Mwanga. Kwahiyo haikutakiwa iwe kama ilivyo. Same ni sawa na Korogwe , Wilaya Kongwe sana nchini zilizodumaa. Tukipata Uhuru Korogwe ilikuwa ''Town council''
 

..wilaya ya Same imedumazwa na kuhujumiwa na serikali na baadhi ya vigogo . Bahati nzuri ni wilaya inayozalisha mpunga, tangawizi, vitunguu, ndizi, hivyo wenyeji wanajiongeza wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…