A
Anonymous
Guest
Sisi ni wakazi wa Magole na Mwanagati, Ilala, Dar es Salaam, tunakabiliwa na changamoto ya daraja linalounganisha maeneo haya mawili.
Awali, Mbunge wetu alifika eneo hilo na kutueleza kuwa daraja hilo limekabidhiwa kwa mkandarasi, ambaye alipewa muda wa miezi 14 kukamilisha ujenzi. Hata hivyo, mpaka sasa hakuna kinachoendelea, na mkandarasi ameondoa vifaa vyake.
Hatujui hatima ya ujenzi wa daraja hilo wala sababu ya mkandarasi kuondoa vifaa. Tunaomba wahusika watoe majibu kuhusu hali ya ujenzi huo na lini kazi itaendelea, kwani daraja hili ni muhimu kwa wakazi wa maeneo haya.