KERO Wananchi wa Misungwi karibu na Wilaya ya Nyamagana tuna shida kubwa ya maji

KERO Wananchi wa Misungwi karibu na Wilaya ya Nyamagana tuna shida kubwa ya maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa miaka mingi, wananchi wa maeneo ya Wilaya ya Misungwi, mkoani Mwanza, yanayopakana na Wilaya ya Nyamagana wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu mkubwa wa huduma ya maji safi na salama, huku mji ukiendelea kukua kwa kasi.

Maeneo yaliyoathirika ni pamoja na Nyanshishi, Nyang'homango na Usagara. Katika maeneo haya hakuna kabisa miundombinu ya mabomba ya maji. Kwa kifupi, si kwamba maji hayatoki, bali hayapo kabisa.

Kutokana na hali hiyo, wananchi hulazimika kutafuta maji kwa shida kubwa na kwa gharama za juu. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba kuna miradi ya ujenzi wa matenki ya maji iliyoanzishwa miaka mingi iliyopita, lakini hadi sasa hakuna dalili ya kukamilika.

Maeneo haya si vijiji bali ni sehemu za mji zinazokua kwa kasi. Hata hivyo, bado hakuna huduma ya maji, wala matumaini ya karibu ya kupatikana kwake kutokana na kusuasua kwa utekelezaji wa miradi hiyo.
 
Tulizoa au tulijua sehemu zenye tabu kama hizo labda diwani au mbunge atakuwa ni wa upinzani. Lakini kumbe ndio walewale chama dume

poleni sana

Inasikitisha sana kwamba tokea uhuru hadi leo tunapambana na madawati, maji wakati miti ipo na vyanzo vya maji vipo karibu

je afya, umeme, usalama, umasikini. changamoto hizo itakuaje kukabiana nazo
 
Back
Top Bottom