KERO Wananchi wa Mtongani Mecco, Kunduchi tumechoka kufungiwa barabara Kila Ijumaa sababu ya mnada

KERO Wananchi wa Mtongani Mecco, Kunduchi tumechoka kufungiwa barabara Kila Ijumaa sababu ya mnada

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wananchi wa Mtongani Mecco, Kunduchi, tunaendelea kupata mateso makubwa kutokana na kukosa njia ya uhakika ya kuingia na kutoka katika eneo letu baada ya kufungwa kwa barabara kufuatia mradi wa DART Phase 4 wa ujenzi wa karakana ya mabasi eneo la Mbuyuni.

Wahusika wa mradi wa DART waliahidi kutoa njia mbadala baada ya kufungwa kwa barabara kuu iliyokuwa inatoka Mbuyuni, lakini hadi sasa wananchi tumebaki tukiwa hatuna njia salama na ya uhakika ya kupita. Barabara ya kutoka Mecco Soko la Zamani hadi Police ndiyo inayotumika kwa sasa, lakini ipo katika hali mbaya sana na haipitiki kwa urahisi.

Kero kubwa zaidi ni kufungwa kwa barabara hiyo kila siku ya Ijumaa kutokana na shughuli za mnada, jambo linalowafanya wananchi wa Mtongani Mecco kuishi kama wako kisiwani bila njia ya kupita.

Hali hii inasababisha wananchi kushindwa kufika kazini, watoto kupata shida kwenda shule, wagonjwa kukosa huduma za haraka pamoja na biashara kuathirika kwa kiasi kikubwa.

Tunaiomba serikali pamoja na viongozi wa mradi wa DART kuchukua hatua za haraka kurekebisha barabara hiyo au kutoa njia mbadala salama na ya kudumu kwa wananchi.
 
Huku hayo yakiendelea mwenyekiti wa serikali ya mtaa ndugu kibele amekuwa dalali wa kuwashawishi wananchi wauze nyumba zao kwa wawekezaji wasiojulikana
Kibele aliyeingia madarakani kwa kuhonga watu bia tunjua kwamba ni mwandani wa diwani wa kata ndugu urio tutaleta faili lake hapa Ili watu wamjue
 
Back
Top Bottom