Lanlady
JF-Expert Member
- Feb 27, 2019
- 1,836
- 6,303
Nimekutana na watu wazima kadhaa wenye ujuzi katika eneo fulani, tatizo kubwa ni kwamba watu hao ni wavivu na tegemezi.
Fikiria unamuita mtu ili akufanyie kazi fulani ambayo utamlipa, halafu mtu huyo anakuomba umlipie nauli ya kuja eneo kazi ilipo.
Hii ni halali kweli? Au ni utegemezi wa kifikra?
Na wakati mwingine unaweza kweli kumlipia nauli na akafika kuanza kazi lakini akashindwa kumaliza kazi hiyo kwa wakati. Kila siku anatoa udhuru. Mara amefiwa, mara mtoto anaumwa. Sababu zinakuwa nyingi.
Iwekwe sheria kali kwa kila mtu mzima kuhakikisha anazalisha na kulipa kodi. Na sio kutegemea ajira za serikalini pekee. Au kutegemea kupokea msaada kutoka kwa ndugu, jamaa au rafiki waliofanikiwa. Huo ni unyonyaji.