Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Poleni sana na Mwaka huu mtapata cha moto zaidi maana hakuna mvua ya kutoshaMheshimiwa Rais popote ulipo, na mheshimiwa Awesso, ni miezi mitatu sasa hatujui maji wakazi wa Ubungo Kibangu mtaa wa Kajima tunaomba msaada wenu viongozi wetu hali ni mbaya sana.
Tuna miezi mitatu hatuna maji
Eneo ni kajima (Rivaside juu) mtaa wa Kibangu Ubungo
Eneo hili ni kubwa kuanzia Novo, kwa mdee, kwa mgogo, Kwa mlacha, kilima cha lami, bonde la kajima, na kwa bondia hii mitaa yote hamna maji kabisa
Mfano, Novo magorofani na mpaka kwa mdee wao wa miezi 6 hawajawahi kuona maji.
Maji hayatoki lakini watu wanauza maji na kuleta na magari na kuyauza kwa ndoo 500
Tumelalamika tumechoka inaonekana kuna mfumo wa watu kula hela na kujineemesha
Kipindi cha Magufuli maji yalikua yakitoka
Sio hivyo tu, wameleta matank ya kuuza maji na inadaiwa na miradi ya mheshimiwa fulani hivi
Naombeni mnisaidie namba ya Aweso tumechoka!!
Hata kama angekuwa nani; mpigeni chini.Mbunge ni kitila