JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Nimeona hii clip, wenyeji wa huko tuambieni kama ishu ina ukweli hii?
======================================
Wakizungumza na Wawakilishi wa Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Vita Rashid Kawawa, Wananchi wa Kijiji cha Mlalamiwa na Matepwende wamedai hawawezi kupokea zawadi za Mbunge wao wakati huduma mbalimbali za Kijamii hazijaimarika.
Viongozi wa Vijiji hivyo walioingia madarakani Novemba 27, 2024 wamesema matumaini yao ni kuwatumikia Wananchi katika matatizo yao ya kijamii yanayowahusu, jambo ambalo pia halijafanywa na Mbunge wao.
Wamesema hayo katika kikao kilichohitishwa na Katibu wa Mbunge Zubery, akishirikiana na Ally Lyuma ambaye ni mpambe wa Kawawa.
Kikao kilifanyika Ijumaa Januari 17, 2025 Saa 1 Jioni katika Kijiji cha Mlalawima, Kata ya Msisima na kuhudhuliwa na Watendaji wa Vijiji vya Matepwende na Mlalawima, Watendaji ni Miraji Haridi na Moyo.
Wenyeviti wa Vijiji ni Kawawa Ally Banda na Athumani Kalumbi Tegi, wengine ni wajumbe wa Serikali za Vijiji hivyo na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka kwenye matawi.
Viongozi hao wa Serikali za Mtaa wanadai miaka mitano inaenda kukamilisha lakini Mbunge wao hajawatumikia Wananchi wa vijiji hivyo kisha anatuma wawakilishi wake kwenda kutoa zawadi ya jezi na fedha jambo ambalo hawaafikiani nalo.
Wanadai hawana huduma ya maji, madarasa ni machache kiasi kwamba Mwaka 2024 kuna shule wanafunzi walifanya mitihani wakiwa chini ya mti, Barabara ni mbovu na hawana huduma ya maji ambapo watu wanakunywa maji ya kisima wakisea pamoja na mifugo.
Wanadai hali hiyo imesababisha Wananchi kukosa imani na Mbunge wao kutokana na kutohudumia vijiji hivyo viwili.
Majibu ya Mbunge ~ Baada ya Wananchi kugomea t-shirt na fedha za Mbunge, ajitokeza na kusema hizo ni fitna za Kisiasa na kuwa wanaichafua CCM
===================================
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Komredi Oddo Mwisho akizungumza na Wanahabari kuhusu masuala ya uongozi leo Januari 23, 2025
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Ruvuma, Komredi Oddo Mwisho akizungumza na Wanahabari kuhusu masuala ya uongozi leo Januari 23, 2025