Wananchi wabomoa nyumba ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kishiri, Nyamagana

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wananchi wenye hasira wa mtaa wa Kishiri huko Nyamagana Mwanza wamebomoa nyumba ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa kwa madai ya kumuua kijana mmoja aitwaye Kinyasi

Inadaiwa mwenyekiti huyo alimkamata Kinyasi kwa madai kuwa aliiba ndala na kumpiga hali iliyopelekea kifo chake.

Haijafahamika mwenyekiti huyo anatokea chama gani.

Source ITV habari!
 
Mkuu wa mkoa kasema huyo dogo alikuwa na record ya uhalifu, lakini amewasema wananchi huku akiruka kusema kosa la mwenyekiti kumuua mtoto.

Source: star tv Habari
 
Hao wanaojua kusoma na kuandika wanaua!!ccm kwann jaman MTU akatishwe ndoto zake
 
Wenyeviti wote wanajulikana walitoka chama gani uchaguzi uleee...
 
Eti haijajulikana ni wa chama gani,kwani si CCM walipita bila kupingwa,serikali za mitaa?
 
Hahaha eti chama gani,mbona iko wazi
 
Ndala, kandambili, malapa ndiyo za kuondoa uhai wa mtu???

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Mkuu wa mkoa kasema huyo dogo alikuwa na record ya uhalifu, lakini amewasema wananchi huku akiruka kusema kosa la mwenyekiti kumuua mtoto
Source: star tv Habari
Kwa hiyo mwenye tabia ya uhalifu mwenyekiti anaruhusiwa kumuua? Huyu mkuu wa mkoa ajitathmini sio anatangulia kutoa hukumu haoni kwamba hapo anamtetea muuaji wakati wananchi wanadai ndio tabia yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…