PostGE2025 Wananchi: Wabunge waache "uchawa" wafanyekazi ya kuwatumikia watanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Kufuatia kuanza rasmi kwa shughuli za Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi jijini Dodoma wametoa wito kwa Wabunge kuachana na tabia ya ushabiki na kusifia kila jambo linalowasilishwa Bungeni, ambapo wameeleza kuwa ni muhimu kwa Wabunge kusimamia haki, misingi ya Katiba na Sheria, badala ya kuunga mkono kila hoja kwa misingi ya kisiasa au kiitikadi pekee.

Wakizungumza na JAMBO TV katika nyakati tofauti, baadhi ya Wananchi hao wamesisitiza kuwa maendeleo ya kweli yatapatikana endapo Wabunge watawajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao, huku wakieleza jukumu la Mbunge si kusifia Serikali kila wakati, bali kuhakikisha maslahi ya Wananchi yanalindwa na sera zinazopitishwa zinawanufaisha wote.

Safi wananchi, wachanwe uchawa sio solution nchi hii
 
Wakizungumza na JAMBO TV katika nyakati tofauti, baadhi ya Wananchi hao wamesisitiza kuwa maendeleo ya kweli yatapatikana endapo Wabunge watawajibika ipasavyo katika kutekeleza majukumu yao, huku wakieleza jukumu la Mbunge si kusifia Serikali kila wakati, bali kuhakikisha maslahi ya Wananchi yanalindwa na sera zinazopitishwa zinawanufaisha wote.
Hao wananchi walipiga kura. Yaani Mtu ashinde kwa jitihada na mbinu zake, then umuelekeze cha kufanya? Maendeleo yataletwa na wananchi wenyewe.
 
Back
Top Bottom