Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Na Mwandishi Wetu
WANANCHI wa Kijiji cha Bulembo, Tarafa ya Kamachumu, wilaya ya Muleba mkoani Kagera wamechangishwa fedha za nguzo ‘hewa’ katika mradi unaotekelezwa na Wakala wa umeme vijijini (REA) kijijini hapo.
Mradi huo unaotekelezwa na REA kupitia kampuni ya Naproi umegubikwa na sintofahamu baada ya kusuasua kukamilika huku wananchi wakichangishwa fedha za nguzo ‘hewa’na kuwasababishia umasikini.
Wafanyakazi wa kampuni Naproi wanadaiwa kuwatapeli wananchi kwa kuwachangisha fedha kwa ajili ya kununulia nguzo kinyume na utaratibu rasmi wa serikali.
Uchunguzi uliofanywa na Pambazuko katika Kijiji hicho, umebaini wananchi zaidi ya 40 wametapeliwa kati ya Shilingi 300,000 hadi 700,000 kutegemea umbali uliopo huku fedha hizo zikiingia mifukoni mwa wajanja wachache bila kutolewa risiti wala maandishi yoyote ya serikali.
Katika uchunguzi huo, wananchi ambao ‘wamelizwa’ fedha zao ni wale ambao hawapo kwenye mpango wa awamu ya kwanza wa kupata umeme wa REA ambao ujenzi wa miundombinu ya mradi huo unaendelea kijijini hapo.
“Mmoja wa familia iliyotapeliwa shilingi 300,000, Akwilina Philemon mkazi wa kijiji hicho alisema, wafanyakazi wa kampuni ya Naproi wakiwa na mmoja wa viongozi wa halmashauri ya kijiji hicho walimfuata na kumweleza kuwa ili aweze kupata umeme awamu ya kwanza anatakiwa kununua nguzo mbili, hivyo atoe shilingi laki sita. Hata hivyo baadaye walikubali kupokea Shilingi 300,000 na kumpelekea nguzo moja.
“Hao vijana wafanyakazi walikuja kwangu wakiambatana na kiongozi tunayemfahamu, walisema wanazo nguzo za ziada, hivyo tukitoa Shilingi 600,000 tutaletewa nguzo mbili na kufungiwa umeme sambamba na wenzetu waliopo kwenye mpango wa awali.
“Niliwaambia walete nguzo tuione ndiyo tutoe fedha. Kweli walileta nguzo hiyo na tukawalipa fedha, lakini baadaye bosi wao alikuja kuichukua akisema hafahamu mpango huo na nguzo hiyo ilichukuliwa kwa mteja mwingine kimakosa.
“Mimi na mume wangu hatukuridhika na hatua hiyo, tulipeleka malalamiko kwenye Serikali ya Kitongoji na Kituo cha Polisi Kamachumu, ambako kijana huyo alikiri na kuahidi kurudisha fedha zetu. Lakini muda unakwenda sioni kinachoendelea na sijui fedha yangu itarudishwa lini, ni maumivu makubwa tumeyapata lakini tunamwachia Mungu”alisema Silichelia.
Mwananchi mwingine, Adroph Simon ameiomba serikali iingilie kati suala hilo kwa sababu limewasababishia hasara na umasikini mkubwa.
Simon alisema yeye aliambiwa umbali wa kutoka kwake panahitajika nguzo mbili, hivyo alipie Shilingi 400,000, hata hivyo aliwapatia Shilingi 300,000 akiahidi kumalizia fedha iliyobaki wakishampelekea nguzo na kuchimba mashimo.
Hata hivyo kama walivyo wananchi wengine hakupewa risiti inayothibitisha malipo hayo, jambo ambalo linadhihirisha kuwa fedha hizo hazikuingia kwenye mfuko wa serikali.
“Hao watu ni kama chuma ulete, walituingia kwa lugha nyepesi ya kutulaghai, kuna dalali wa hao wawekaji wa miundombinu ya umeme hapa kijijini ametumika kwenye wizi huo.”alisema Simon.
Aidha uchunguzi umebaini kijijini hapo umebaini kuwapo udhaifu wa usimamizi pamoja na uhaba wa vifaa vya kufanyiakazi katika kutekeleza mradi huo ambao hadi sasa haujulikani utakamilika lini.
Pia hakuna uwazi kuhusu mipaka ya kazi za kitaalamu na zile zinazotakiwa kufanywa na vibarua wa mkandarasi au wananchi wenyewe.
Mathalani, baadhi ya maeneo ya ardhi ya hicho yana mwamba, hivyo vinahitajika vifaa maalum vya kuchimbia mashimo ya kusimika nguzo. Hata hivyo wananchi ambao maeneo yao yana changamoto hiyo wanalazimishwa aidha kuchimba mashimo wenyewe au walipie Shilingi 5000 kwa ajili hiyo.
Jambo hilo limeibua mkanganyiko na unyanyasaji mkubwa hususani kwa wananchi ambao ni wazee wasiokuwa na nguvu za kuchimba mashimo hayo na wale wasikuwa na fedha za kuwalipa wachimbaji.
“Sisi tusiokuwa na uwezo wa kuchimba mashimo au hatuna fedha tunaambiwa tujiongeze, wanatutisha kuwa nguzo zilizowekwa katika maeneo yetu zitahamishwa, hatuna amani na huu mradi”alisema mmoja wa wananchi hao ambaye hakutaka jina lake liwekwe gazetini.
Wakati hayo yakiendelea, madai ya nguzo kuhamishwa kwenda maeneo tofauti yamejitokeza pia katika Kijiji cha Bulamula Kitongoji cha Bushaka, Kata Kamachumu ambapo wananchi zaidi ya 40 wanadai walipimiwa maeno yao miezi mitatu iliyopita kwa ajili ya kupelekewa umeme wa REA, lakini mpaka sasa hawajui nini kimekwamisha.
Alizungumza kwa niaba ya wenzake, Didas Mtimagwe ameliambia Pambazuko kwa simu kuwa licha ya danadana kadhaa wameshuhudia nguzo ambazo waliahidiwa kuletwa kwenye eneo lao zikipelekwa kitongoji jirani cha Mbale, hivyo ameiomba serikali kuingilia suala hilo kwani wanahisi kuna mchezo mchafu unandelea.
Akizungumza kwa niaba ya Mhandisi Mkuu wa REA Mkoa wa Kagera, Bagasha Laurent alisema Ofisi yake haina taarifa za wananchi kuchangishwa fedha kwa ajili ya nguzo na kwamba jambo hilo kama limefanyika ni kinyume cha sheria na taratibu za uwekaji umeme vijijini.
“Taarifa hizo sisi hatuna, na nimekuwa nikiwasiliana na diwani wa eneo hilo kila mara lakini hajanipa taarifa wala malalamiko hayo, kimsingi sio sheria kumchangisha mwananchi fedha kwa ajili ya uwekaji umeme kupitia REA, hizi ni fedha za Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. Taarifa hii naipokea na tunaifanyia kazi mara moja” alisema Bagasha.
Kuhusu kuwalazimisha wananchi kuchimba mashimo ya kuweka nguzo, Bagasha pia alishtushwa na suala hilo, ambapo alisema hilo ni kosa na sio utaratibu kwani mwananchi hawajibiki kuyachimba kwakuwa hiyo ni kazi ya fundi aliyepewa kazi hiyo.
“Kuhusu mradi kutokukamilika kwa wakati hii ilitokana na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja na fundi mkuu aliyepewa kazi hiyo awali aliugua, tumepeleka mwingine. Pia kuchelewa kwa mradi husika kunategemea vitu vingi ikiwamo ukaguzi wa kila hatua inayofanyika.
“Kila hatua lazima ikaguliwe ili kujiridhisha kama imefanyika kwa viwango, hata uchimbaji wa mashimo na usimikaji wa nguzo lazima vikaguliwe kabla ya kuendelea na hatua inayofuata”alisema Bagasha.
Awali, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Bulembo, Erickson Josephat alikiri kupokea taarifa za wananchi kuchangishwa fedha kwa ajili ya kupelekewa nguzo za umeme.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Mathias Msigei alisema jambo hilo limefika ofisini kwake kwa kuchelewa.
“Ni kweli jambo hili lipo, lakini limefika ofisini kwangu kwa kuchelewa, bahati mbaya waliokuja kwangu kulalamika tayari walikwisha tapeliwa fedha zao.”alisema Msigei.
Kwa upande wake, Kaimu Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera, Ezekiel Sinkala alisema wanafanyia uchunguzi suala hilo kwa sababu miradi yote ya umeme wa REA mwananchi hapaswi kuchangishwa chochote zaidi ya kulipia shilingi 27,000 ambayo ni bei elekezi.
“Tunafuatilia suala hilo kwa uchunguzi zaidi kwa sababu miradi yote ya umeme wa REA inagharamiwa na serikali, mwananchi hapaswi kuchangishwa chochote zaidi ya shilingi 27000 tu kwa maeneo yote ya vijijini”alisema Sinkala.