Bikis
Member
- Feb 23, 2019
- 52
- 74
Mhe Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Mama Samia Suluh Hassan, wakati wa kuwapisha makatibu wakuu na baadhi ya wakuu wa taasisi mbalimbali za serikali aliagiza wizara ya maliasili na utalii inayongozwa na mhe.Dr Damas ndumbaro(MB) watafute suluhisho la kudumu ndani ya wenyeji waishio ndani ya mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro.
Lakini badala ya wizara kushirikisna na wadau mbalimbali na wenyeji hao kuanza majadiliano huru ya namna bora ya kupata suluh,, lakini Mamlaka ya ngorongoro imetoa agizo la siku 30 kwa wenyeji waliojenga ndani ya vijiji vyao wabomoe nyumba zao kwa mikono yao wenyewe, jambo lilizua taharuki kubwa kwa wananchi waishio ndani ya ngorongoro.
Siku ya tarehe 16 april 2021 waziri Ndumbaro kupitia kwa mhe.mbunge wa jimbo la ngorongoro ambaye ni naibu waziri katika ofisi ya waziri mkuu uwekezaji aliomba kuonana na baadhi ya viongozi wa kimila, madiwani na baadhi ya wawakilishi kutoka kata mbalimbali ili wajadili namna ya kuanza kujenga msingi wa ushirikiano katika kutafuta suluhu la kudumu juu ya uhifadhi na maslahi ya wenyeji wa mamlaka waishio ndani ya mamlaka kisheria.
Chakushangaza magari ya mamlaka ya hiyo iliwasomba ya viongozi wa wenyeji hao na kufika karibu na makao makuu ya ngorongoro kwa lengo la kuonana na mhe.waziri laki ndumbaro kabla ya kuongea na wenyeji hao alifika kwenye ofisi ya mamlaka ya Ngorongoro na kupokelewa na mwenyeji wake Dr.fredy Manongi mhifadhi wa ngorongoro na baada ya majadiliano ya mda mfupi waziri alishauriwa arudi Dodoma na asiongee na wenyeji hao eti kwa taarifa za kiintelijensia.
Jambo hilo liliwapelekea wenyeji kulalamika juu ya waziri kuchoma mafuta kutoka makao makuu ya nchi Dodoma na kushindwa kuonana na wenyeji, na wamasai hao walilalamika kwamba hizo ni mbinu ya mara zoote ya mamlaka ya ngorongoro kuwahujumu mawaziri na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu za serikali kila wanapopanga kushirikisha wenyeji katika kutafuta suluhu la kudumu(wenyeji walisema NCAA hawakutaka waziri ajue ukweli kupitia kwa wananchi hao waliokesha kumsubiri kwa lengo la majadiliano)
Kwa maoni ya wenyeji, mhe mbunge, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya, na mwenyekiti wa wenyeji waishio ndani ya mamlaka hiyo na baadhi ya viongozi wa mila kwa pamoja walikiri kuomba serikali ya mama samia suluhu kuingilia suala hilo, na kwamba wenyeji wapo tayari kwa asilimia 100 kushirikiana na serikali yake kutafuta suluhu ya kudumu ndani ya ngorongoro kwa maslahi ya sasa na kwa kizazi kijacho.
Wananchi wote wamekiri tangu alipoteuliwa ndugu Manongi mahusiano kati ya wananchi na taasisi hicho imekuwa ni changamoto kubwa sana.
Wananchi waliilamikia kamati iliyoteuliwa na aliyekuwa katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii prof mkenda wakisaidiana na bwana Manongi chini ya ufadhili wa mamlaka hiyo ilikataa katu katu kuchukua maoni ya wenyeji hao...
Na kwamba maoni yote yaliyo katika report hiyo haina maoni hata moja ya l wananchi jambo ambalo siyo afya kwa nchi yetu kwa ujumla..
Zaidi ya mabilioni ya pesa za ncaa zilitumika kuandika report nyingi zinazowachafua wananchi hao kwamba ndio waharibifu wa mazingira ya mamlaka hiyo.
Wananchi waliongea juu ya ujenzi wa majengo mengi ya mamlaka hiyo, mahoteli makubwa, na lodges pamoja na idadi kubwa ya waajiriwa wa zaidi ya 800 ilihali kuna wenyeji wenye sifa hizo lakini hawapewi fursa hiyo kutokana na chuki binafsi ya dr.manongi na wenyeji hao!!
Wananchi walizungumzia suala lao la kuhamisha kutoka Serengeti kati ya miaka 1959 kuja ndani ya mamlaka ya HIFADHI hiyo kwamba ilikuwa ni jambo la makubaliano na kama leo tena tunatolewa kwenye sehemu tuliyoletwa 1959 basi tunahitaji kushirikishwa ili na sisi tutuoe maoni yetu juu ya mustakabali wa maisha yetu na watoto wetu.
Baadhi ya wenyeji wamekiri ni kweli kuna changamoto la uongezeko la watu lakini siyo kweli kwamba wamekuwa waharibifu wa mazingira kama ncaa inapotumia nguvu kubwa ya pesa na ushawishi kuiaminisha serikali na watanzania kwamba wananchi hao wamekuwa kero.
Wamezungumzia juu ya watalii zaidi ya mil moja wanaotembelea ndani ya mamlaka hiyo, crater ya ngorongoro kupokea magari mengi kuliko uwezo wake kwamba ndio sababu kubwa ya changamoto katika ecology ya hifadhi hiyo
Kwa wenyeji wachache waliojenga makazi ya kudumu ni chini ya asimilia 1% ya wenyeji wote.