Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 9,140
- 15,963
Wananchi wa kijiji cha Lemanda,oldonyo sambu wanakabiliwa na Njaa kutokana na Kukosekana kwa mvua muda mrefu na hivyo kupelekea mifugo kufa na wanafunzi kuanguka shuleni kutokana na njaa.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Mosses Nguluma amesema kuwa eneo hilo lipo ukanda wa chini na hivyo hupelekea Kukosekana kwa mvua mara nyingi. Na hivyo ni muda mrefu hawajapata mavuno katika mashamba yao. Kwani shughuli yao kubwa ni kilimo na ufugaji.
Pia mwenyekiti huyo amesema kuwa hali hiyo imepelekea wanafunzi shuleni kudondoka kutokana na Njaa nakuwa wazazi hushindwa kulipa gharama za chakula mashuleni, hivyo basi mtoto anaenda shuleni akiwa na njaa na shuleni pia hushinda na njaa.
Kutokana na hali hiyo ya ukame imewalazimu wanaume kuondoka nyumbani na Mifugo yao na kupeleka maeneo ya mbali kwa ajili ya kuwataftia malisho ya majani na hivyo kuwaacha akina mama na watoto peke yao wakiteseka.
Baadhi ya Wakina Mama wa kijiji hicho wameiangukia serikali iangalie namna ya kuwasaidia kwani wamekuwa wakiteseka na watoto kutokana na kuwa wanategemea mifugo na kilimo tu kwani ni mara kwa mara eneo hilo hukumbwa na njaa na sababu kubwa ikitajwa ni kuwa eneo hilo lipo ukanda wa chini wa mvua hali inayopelekea mara nyingi mvua kunyesha Chini ya kiwango