Wananchi wakazi wa Kunduchi kuandamana hadi kwa RC Makonda kupinga Serikali ya mtaa kuwachangisha 100,000/= kila mmoja kujenga mtaro!

Wananchi wakazi wa Kunduchi kuandamana hadi kwa RC Makonda kupinga Serikali ya mtaa kuwachangisha 100,000/= kila mmoja kujenga mtaro!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wakazi wa Kondo maeneo ya Mwaitenda na Bunge st katika kata ya kunduchi wilayani kinondoni wamepanga kuandamana hadi kwa RC Makonda kupinga serikali yao ya mtaa kuwachangisha michango kinyume cha utaratibu.

Wakazi hao wamedai serikali ya awamu ya 4 wakati Makonda akiwa DC wa Kinondoni ilishatoa fedha za ujenzi wa mfereji wa kupeleka maji hayo baharini baada ya Rais Kikwete kutembelea eneo hilo.
Sasa wanashangaa iweje tena waanze kuchangishwa kiasi kikubwa cha fedha bila kuwepo kikao chochote cha wananchi?

Wananchi hao wameitaka CCM kuwa makini kwani huu ni mwaka wa uchaguzi.

Source: Global

Maendeleo hayana vyama!
 
Taarifa yako haijajitosheleza weka link ya video au picha siyo kuishia kutuambia source global. Global ipi?
Global tv?
Global alliance?
Au Global link?.

Ok any way Subiri waliopiga kura za wenyeviti wa mtaa waje.
 
Wachangie maana hakuna namna awamu hii ya 5 serikali haina fedha bali wanajimwambafai na kununua ndege na kupika takwimu uchumi unakuwa wakati unaporomoka kwa kasi mbaya
 
Wachangie maana hakuna namna awamu hii ya 5 serikali haina fedha bali wanajimwambafai na kununua ndege na kupika takwimu uchumi unakuwa wakati unaporomoka kwa kasi mbaya
Halafu eti mbunge wao ni Halima Mdee!
 
Taarifa yako haijajitosheleza weka link ya video au picha siyo kuishia kutuambia source global. Global ipi?
Global tv?
Global alliance?
Au Global link?.

Ok any way Subiri waliopiga kura za wenyeviti wa mtaa waje.
Mbona povu au uko kwenye Kamati ya Uchangisha Jamaa Anapeperusha dili kua Dirisha
 
Back
Top Bottom