Wananchi wamtimua Mwalimu "Freemasons" Wilayani Busega Mkoani Simiyu.

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,258
Reaction score
1,416
Vituko haviishi bongo,

Wananchi wilayani Busega mkoani Simiyuwametaka kuondolewa kwa Mwalimu mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja kwa madai kuwa ni "Freemasons".

Wananchi hao wamefikia hatua hiyo baada ya kutokea "ugonjwa wa ajabu" wa kuanguka anguka kwa wanafunzi katika shule ya sekondari Mwamagisisi.
Wanafunzi wengi katika shule hiyo wameonekana kupata matatizo ya kuanguka ovyo kila wakati jambo ambalo wanachi wamelihusisha na imani za kishirikina huku wakidai kuwa "TV asili" zinaonesha kuwa Mwalimu tajwa ndiye "anayewachezea" wanafunzi hao hadi kupelekea kupata matatizo hayo ya kuanguka ovyo.

Wakizungumza kwenye mkutano maalum wa wazazi na viongozi wa shule juu ya tatizo hilo wananchi wengi walimtuhumu Mwalimu huyo kuwa ni Freemasons na hivyo kutaka aondolewe.

Afisa Elimu wa wilaya hiyo amesema atamwamisha mwalimu huyo ili kuwaridhisha wananchi lakini hakubali kamwe kuwa mwalimu huyo ni freemasons.

Wakielezea sababu za matatizo yanayowapata wanafunzi shuleni hapo, wataalamu wamedai kuwa hiyo inatokana na lishe duni, uchovu na njaa na wala si sababu za ushirikina na u-freemasons kama wananchi hao wanavyoamini.

...Duniani kuna mambo!
 
Hivi hii falsafa ya freemasons wa TZ wanaielwa kweli maana kila siku nasikia huyu mjenzi huru , atakuwa mjenzi huru ni mjenzi huru naona kama tunakurupuka sana na tumejaa uzushi mwingiii!
Na nadhani ni only in TZ ambako wajenzihuru ni masikini!
 
Mkuu Mkeshaji ebu angalia hilo jina la shule ndo lenyewe kweli?
 
Last edited by a moderator:
hiyo kwa Wasukuma sitashangaa hata kidogo

kesho kusikia mwalimu ameuawa kwa tuhuma za

ushirikina
 
aliyekuwa anatoa majibu ya tv ya asili hakuwa na ugomvi wowote na mwalimu husika?
 
Matatizo kama hayo hutokea nchi masikini na fukara sana, kila kitu kwao ni uchawi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…