JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Baadhi ya wananchi Wanaotakiwa kupisha Ujenzi wa Bandarikavu katika eneo la Nandanga, Kata ya Mpemba, Halmashauri ya Mji wa Tunduma, Mkoani Songwe wameilalamikia Ofisi ya Serikali ya Mtaa kushindwa kuwashirikisha katika hatua za Mchakato wa kulipa fidia na kuandikisha watu wasiohusika kwa lengo la kuwalipa fidia.
Wananchi hawa Wanadai Serikali ya Mtaa inahujumu Mchakato wa ulipaji wa Fidia katika eneo hilo kwa kuweka watu wasiohusika, huku wakienda mbali zaidi kuiomba Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kuingilia kati kwa kuitisha mikutano ya hadhara ya kusikiliza kero zao.
TIPSONI NZUNDA Mkazi wa Nandanga. AIZACK MWAMPASHI Mkazi wa Nandanga, HAMIS MSUKWA mkazi wa Nandanga LANGBOSS SICHONE Mkazi wa nandanga wanaelezea
Upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, ELISHA MSOMBAanakiri kukosekana kwa nyaraka za umiliki wa maeneo haya wakati wa uhakiki huku anaeleza utaratibu uliotumika.
Licha ya kuishukuru serikali kwa kutoa zaidi ya Bilioni 7 kwaajili ya kulipa fidia kwa wananchi zaidi ya 300 katika mitaa ya Msinde na Nandanga, Diwani wa kata hii, JIMMY MTAWA anasema hajapokea Malalamiko ya Wananchi.
Chanzo: EATV