Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA DAR, PWANI ZASISITIZA ULINZI WA VYANZO VYA MAJI
Na Crispin Gerald
Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani zimeonya vikali wananchi wanaoharibu vyanzo vya maji na kusababisha uharibifu kwenye mfumo wa maji.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea vyanzo vya uzalishaji maji vya Ruvu Juu na Ruvu chini Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makala amewataka wananchi kuacha uharibifu wa vyanzo vya maji kwa kufanya shughuli zinazosababisha uhaba wa maji kwenye mfumo.
"Mimi na wajumbe wa Kamati tumetembelea na tumejidhirisha pasipo shaka kwamba hali ya upatikanaji wa maji kwa Dar na Pwani ni ya kuridhirisha, na hii ni matokeo ya kazi kubwa iliyofanywa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)," amesema.
Ameongeza kuwa jitihada hizi zinapaswa kuungwa mkono na viongozi wote wa Ulinzi na Usalama na wananchi kwa ujumla katika kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa na kutunzwa ili huduma iwe endelevu.
Mhe. Makala amesisitiza kuwa wananchi wote waliopitiwa na vyanzo vya maji waache tabia ya kuchepusha na kuharibu vyanzo vya maji na ambao hawana vibali.
"Mbali na hapo tuna wajibu wa kuendelea kufanya maombi ili mvua za Vuli zinyeshe ili maji yaendelee kupatikani kwani kwa sasa bado tunategemea mvua," ameeleza Mhe. Makala.
Amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya uwekezaji mkubwa wa fedha kwenye sekta ya maji, hivyo Kamati zote za Ulinzi na Usalama zinawajibu wa kuhakikisha vyanzo vyote vya maji vinalindwa ipasavyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge amesema kuwa kulingana na viashiria mbalimbali vilivyotolewa vya hewa juu ya uwepo wa uhaba wa mvua kwa mwaka huu, kuna kila sababu ya kuchukua tahadhari mapema ili kuepuka athari zilizojitokeza mwaka jana wakati wa ukame.
"Hivyo Mamlaka ya Bonde inapaswa kujipanga vizuri kuhakikisha vibali vinatolewa kulingana na vipaumbele, lakini pia kusitisha shughuli za kilimo za wananchi zinazosababisha uharibifu wa vyanzo vya maji," amesema Mhe. Kunenge.
"Hivyo Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa yote zinapaswa kuhakikisha zinawadhibiti wale wote wanaosababisha uchepushwaji wa maji kwenye vyanzo vya maji," ameeleza.
Niwatake wakazi wa Pwani na Dar es Salaam kwa ujumla kuwa watunzaji wazuri wa vyanzo vya maji kwa kuwa DAWASA inafanya kazi kubwa ya kuzalisha na kusambaza maji kwa wananchi.
Akitoa maelezo ya hali ya upatikanaji wa maji Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema kuwa lengo la ziara ni kuonesha hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Mamlaka katika kuokoa ukame ulitokea mwezi wa tisa na kumi mwaka 2021.
"DAWASA tumejitahidi kujenga Bwawa kwenye chanzo cha kuzalisha maji cha Ruvu chini kwa lengo la kuweka hifadhi ya maji itakayowezesha maji kupatikana muda wote hata kipindi cha ukame," ameeleza Mhandisi Luhemeja.
Ameongeza kuwa kikubwa tunaomba viongozi wa Kamati za Ulinzi watusaidie kuwadhibiti watu wanaochukua maji kwenye vyanzo vya maji na kusababisha shida kwenye mfumo, kazi hii inatupa imani ya uhakika wa maji kwa kipindi chote hata kwenye ukame.