Magufuli 05
JF-Expert Member
- May 7, 2023
- 1,433
- 2,791
Jeshi la Polisi kwanini mmezuia? Ni haki ya wanaoandamana kama ilivyohaki ya wanaondamana kupongeza juhudi za serikali. Kwanini hawa huwa mnawaruhusu?
Kwani familia zenu zipo Uarabuni au Zimbabwe?
Mkataba ule utatuliza wote mimi na nyingi na Watanzania wote wakati Rais Samia atakuwa kastaafu na kazeeka. Hivi mpangaji anaweza kumpa masharti mpangishaji (mwenye nyumba) kiasi kile? Pengine nanyi mmeona mapungufu lakini mnaogopa kulinda tu nafasi twenu. Huo ni uoga.
Watoto wenu, wajukuu wenu na vizazi vyenu vitakuta Tanzania ya hali gani? Kwa masharti yale tuna mashaka na DP kama ni wawekezaji wenye nia nzuri, hivyo waachieni Watanzania wafikishe ujumbe kwa wahusika.
Tambueni kwamba ni sisi tuliwachagua na kuwapa mamlaka hayo. Tusipowaelewa tuna haki ya kuwapinga hadharani kwa mstakabali wa nchi yetu. Wakishupaza shingo leo, uchaguzi unakuja watatupigia magoti na kutubembeleza nasi tutawakataa kwenye sanduku la kura.
Chonde chonde Afande IGP na wasaidizi wako waacheni Watanzania wenye sauti wawa wakilishe wasio na sauti. Mkiwazuia wenye nchi yao kuitetea, Mwenyezi MUNGU atawauliza siku za mwisho wa uhai wenu.
Mungu ibariki Tanzania 🇹🇿