Wananchi Waongeza Kasi ya Ujenzi wa Sekondari Mpya Kwenye Kata za Jimbo la Musoma Vijijini

Wananchi Waongeza Kasi ya Ujenzi wa Sekondari Mpya Kwenye Kata za Jimbo la Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

WANANCHI WAONGEZA KASI YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA KWENYE KATA ZETU

Jimbo la Musoma Vijijini linaongeza kasi ya ujenzi wa sekondari mpya za Kata kwa kushirikiana vizuri na Serikali yetu.

Vilevile, kasi imeongezeka kwenye ujenzi wa maabara tatu (3) za masomo ya sayansi (physics, chemistry & biology laboratories) kwenye kila sekondari ya Kata

Mabadiliko mapya ya mfumo wa elimu nchini mwetu, yatahitaji ongezeko kubwa la shule za sekondari.

Mabadiliko hayo ni kwamba wanafunzi wa shule za msingi watasoma hadi darasa la sita (Std VI), na wote wataendelee kupata elimu ya sekondari hadi Kidato cha Nne (Form IV).

Idadi ya Sekondari Jimboni mwetu
(Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374)

(i) Sekondari za Kata/Serikali: 26
(ii) Sekondari za Madhehebu ya Dini: 2

Idadi ya Sekondari zenye Kidato cha V & VI
(High Schools)

(iii) Kasoma High School
Inafundisha masomo ya "arts" pekee

(iv) High Schools mbili (2) zimepata usajili wa kufundisha masomo ya sayansi. Hizo ni Suguti & Mugango High Schools - maabara 3 za masomo ya sayansi zipo na mabweni yapo

Jimbo letu linaongeza kasi ya ujenzi wa sekondari mpya kama ifuatavyo:

I - Ukamilishaji wa sekondari zilizoanzwa kujengwa (miaka kadhaa iliyopita) na wananchi wakishirikiana na viongozi wao.

Fedha za Mfuko wa Jimbo zinachangia ujenzi huu

Sekondari mpya hizo zinajengwa vijijini: Kisiwa cha Rukuba, Muhoji (Serikali imeanza kuchangia) na Nyasaungu

Idadi: Sekondari mpya tatu (3)

II - Sekondari mpya zinazoanza kujengwa mwaka huu kwa kutumia michango ya fedha na nguvukazi za wananchi na viongozi wao

Vijiji vinavyojenga ni: Chitare, Kataryo, Kiriba, Mmahare, na Nyambono

Idadi: Sekondari mpya tano (5)

III - Sekondari mpya zinazojengwa kwa fedha za Serikali na wananchi wamekubali kuchangia nguvukazi

Vijiji vinavyojenga ni: Butata, Kasoma na Kurwaki

Idadi: Sekondari mpya tatu (3)

Taarifa za ujenzi wa kila sekondari zitatolewa.

WANA-MUSOMA VIJIJINI TUENDELEE KUCHANGIA UJENZI WA SEKONDARI MPYA JIMBONI MWETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumamosi, 24.8.2024
 
Back
Top Bottom