Wananchi watahadharishwa upandaji maua kiholela, yaelezwa kuna maua yenye sumu

Wananchi watahadharishwa upandaji maua kiholela, yaelezwa kuna maua yenye sumu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Msimamizi wa kituo cha Taifa cha kudhibiti matukio ya Sumu (NPCC) iliyopo katika Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali(GCLA) Yohana Goshashy ametahadharisha jamii kuacha kupanda maua majumbani kiholela badala wake wawaone wataalamu ili aweze kuwaonesha maua ambayo hayana madhara.

Wakati wa mahojiano maalum na HabariLEO, Goshashy alisema yapo baadhi ya maua ambayo yanasumu ambazo zinaweza kusababisha madhara ikiwemo kifo.
Yohana Goshashy.jpg

Amesema sumu ya baadhi ya mimea yanaweza kusababisha mzio kwa watoto hasa wakigusisha na sehemu kama macho na mdomo wanaweza kuwashwa macho na midomo kuvimba, wengine kulazwa hospital na wengine kupoteza maisha endapo wakitafuna mbegu za maua husika.

“Maua yanapokuwa karibu na nyumba au kupandwa ni vyema wakajua tabia husika ya maua wakati wanapopanda na waone umuhimu wa kuangalia watoto wakati wa kucheza wasije kukumbana na matukio ya sumu kwasababu baadhi ya maua yanasumu.

Ameongeza “Kila anayepanda maua nyumbani ahakikishe ni salama kuna watu wanajua mambo ya maua na miti lakini hata wakitupigia tunaweza kumwonesha maua hatarishi na kuchukua tahadhari.

Amesema miongoni mwa maua ambayo yanaweza kysababisha madhara yanajulikana kwa jina la Mnyonyo ambao unasumu inayoweza kusababisha kifo.

“Maua hayo mengi yanamajina ya kisayansi lakini kuna mmea wa kawaida ambao wengine wanatumi kwa tiba pia na urembo yanaitwa mnyonyo yanasumu ambayo yanaweza kupelekea kifo.

”Cha msingi ni mtu kujua aina ya maua ambayo anayo nyumbani kwakwe kuna yenye sumu ila ukiwa na ufahamu utachukua tahadhari kuna mengine yanafanana na Mkonge huwa yanasumu pia,”amesisitiza.

Amewashauri jamii kuwa ni vyema kupanda mboga badala ya maua ili kupata chakula.
 
Kuna maua mengine ukiyagusa yanasinyaa ghafla, baada ya muda yanarudi hali yake ya awali. Kuna mengine yana utomvu kama minyaa unashangaa hayo maziwa yana usalama gani kama mtu atayagusa ? Maua mengine yanavutia wadudu wakorofi
 
Hii elimu kuhusu maua inabidi itolewe kwani watu wengi hawajui kama kuna maua yenye madhara. Mimi naamini hakuna mtu atakayepanda maua ambayo ni hatari kwake na kwa familia yake.

Hawa wataalamu wangesema ni maua gani yenye sumu ili watu wayajue, hilo la kusema mpaka wapigiwe simu ndo wawaeleze watu ni maua gani yanafahaa haitasaidia sana.
 
Hii elimu kuhusu maua inabidi itolewe kwani watu wengi hawajui kama kuna maua yenye madhara. Mimi naamini hakuna mtu atakayepanda maua ambayo ni hatari kwake na kwa familia yake.

Hawa wataalamu wangesema ni maua gani yenye sumu ili watu wayajue, hilo la kusema mpaka wapigiwe simu ndo wawaeleze watu ni maua gani yanafahaa haitasaidia sana.
Hii ndio sawa.Nimewahi kuona nyumba moja wamepanda haya maua yanafanana na mkonge na kuna watoto,alipita mtu njia hapo,akawafahamisha hao wenye nyumba kuwa huu mmea una sumu,ikateni,wenye nyumba waliikata mda ule ule.
Sikumbuki uko vipi huo mmea,kwa hiyo elimu ni muhimu,watu wapewe.
 
Labda na sisi tumpe ushauri mzuri wa utekelezaji kuliko alivyosema;
Ukifuatilia utaona kuwa, miti ya maua inayotumiaka kwa wingi majumbani haifi hata mia (species)
Nashauri wawe na ukurasa watakaoweka picha za maua ambayo ni hatarishi ili watu wapate ujumbe kwa haraka au Pengine, wawe na namba za whatsup ambazo mtu anaweza kutuma picha na kupata ushauri bure.
Tofauti na hapo alichokiandika ni kama hakitekelezeki kwani sijui kama wanavituo vingapi nchi nzima wanavyotegemea watanzania waende huko kupata ushauri...
 
Hivi kuna mtu alishawahi kufa kwa sumu ya maua??
 
Acha basi kupotosha
Kinachowadhuru watu sio maua bali sumu zinazotumika kwenye maua
Najua nachokiongea yapo Maua yana sumu na dawa zinazotumika kutunza maua ni sumu pia mbona nimeandika kwa urahisi sana kuelewa shida nini?
 
Kina maua mengine yanatabiri kifo Cha Bab kuanza Kabla ya mama
 
Back
Top Bottom