Wananchi wataharuki yanayoendelea Mabibo Jeshini

Wananchi wataharuki yanayoendelea Mabibo Jeshini

CHIZI VITABU

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2021
Posts
1,061
Reaction score
2,477
Niko na jamaa yangu hapa maeneo ya Grocery ya Manka nakula double kick huku nikipiga story na wadau, kuna mdau mmoja mida ya mchana leo alikuwa mitaa ya mabibo anatupa mchapo wa ajabu kidogo

Inasemekana juzi kuna Askari Polisi alienda mitaa ya Mabibo Jeshini kwa wakurya kukamata gongo akapigwa mapanga huku akipigiwa kelele za mwizi sasa leo ni vava voom zito defender zinakamata watu hovyohovyo bodaboda wanakimbizwa na polisi wakitelekeza zinatobolewa matairi kwa hasira

Kwa mujibu wa mtoa story polisi wanakamata Mabibo kwa juu ila tukio limetokea jeshini huko chini kwa wakurya, kuna raia mwema alikuwa amepaki pikipiki yake nje kaingia ndani kwake kutoka anakuta tairi zimepasuliwa kaongea maneno ya uchungu na kujiapisha viapo vya ajabuajabu

Nawasilisha kama nilivyosikia hapa grocery kwa manka, nawasalimu kwa jina la double kick
 
Si waende huko kwa wajeshi wakurya watoboe hzo pkpk zao
FB_IMG_16271979214214635.jpg
 
  • Thanks
Reactions: K11
Back
Top Bottom