Abraham Lincolnn
JF-Expert Member
- Apr 12, 2018
- 2,754
- 4,975
Kiongozi wa nchi anapohangaika kufurahisha magenge na wanasiasa kwa lengo la kujinasibu kisiasa na kusahau majukumu na kazi ya kiongozi wa nchi ni yapi, si dalili njema kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi kwa taifa lolote.
Unapohangaika kufurahisha vikundi vya watu ni wazi kwamba kamwe hautafanikiwa kukamilisha kufurahisha kila mmoja kwa 100% na ukizidi kulazimisha kukubalika miongoni mwa watu unakuwa mtumwa wa kuhangaikia kuwafurahisha watu badala ya kutekeleza majukumu ya msingi ambayo yatakuwa kielelezo cha ufanisi wako katika kazi na kuacha watu wapongeze wenyewe.
Maendeleo ya nchi hayaji kwa porojo za jukwaani na kufurahisha makundi ya watu bali kwa jasho na damu, kwa kuchapa kazi, kuweka sera bora za maendeleo na kuzisimamia kwa ukamilifu n.k angalia mfano wa China, hawakupata maendeleo waliyonayo kwa porojo za jukwaani.
Kiongozi wa nchi anayetumia muda wake mwingi kufurahisha watu kwa malengo ya kunufaika kisiasa na kusahau wananchi ambao mpaka sasa wanahangaika na mgao wa umeme,maji n.k HAFAI HATA KIDOGO!
Leo hii Tanzania hakuna mipango wala mikakati mikubwa ya maendeleo.Miradi mikubwa kama SGR, JNHP na mashirika makubwa kama ATCL yanaelekea kufa kutokana na usimamizi mbovu na viongozi kugeuka wanasiasa wa kufurahisha magenge na kuzungumzia petty issues ambazo sio kipaumbele kwa nchi masikini kama Tanzania.Hakuna mikakati na focus ya jumla kama taifa, huku viongozi wakichoma mamilioni kwenda kuhudhuria mkutano kujadili athari ya gesi ya ukaa!
INASIKITISHA SANA