Tarehe 2 Jan. 2007, kuna kijana mmoja kwa jina la Prosper alifanya kitu North Mara ambacho sidhani kama kuna mtanzania amefanikiwa kufanya. Kwa maoni yangu ingebidi apewe nishani ya ushujaa. Lakini sidhani kama story yake ilisikika. Lakini kwa kuwa inahusiana na hii, naomba niwakilishe.
Prosper alifukuzwa kazi na mwenzake mwingine, tumuite Peter, kwa kosa la kushiriki kuiba mafuta katika magari ya kazi. Kila mtu mgodini, alikuwa anajua haiwezekani Prosper alishiriki kwa sababu ni kijana tofauti kabisa na wenzake wengine mgodini. Mpaka Peter mwenyewe, ambaye alikubali alifanya hilo kosa, alikiri Prosper hakuhusika. Na kila mtu alikuwa anajua Prosper haibagi mafuta kabisa, kwa sababu ndivyo alivyo.
Lakini kwa sababu wazungu ni Mungu mtu kule, basi huyo mzungu aliyewasemea akachukuliwa anaongea ukweli tupu, na akasikilizwa kama kawaida, vijana wakapewa summarily dismisal, bila lipo lolote. Ilikuwa ni kawaida kwa wabongo kufukuzwa bila sababu za msingi na bila kupewa haki zao, ilimradi tu kuna mzungu kamsemea.
Prosper alijaribu sana kuomba haki yake lakini hakusikilizwa. Akafanikiwa kupata mtu wa kumlengesha kwa meneja wa mgodi ili aelezee side yake ya story, meneja akasema hana time.
Baada ya kuchoka, kijana prosper akaenda mgodini akawaambia walinzi anaenda Mwanza, atarudi baada ya siku 3 kuchukua hela yake, kwa hivyo wamtayarishie. Kwa kuwa Prosper ni kijana mpole mno ni rahisi sana kudharau kauli zake, hawakugundua kwamba kijana hasira ilikuwa ishamzidi kimo.
Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya tatu. Asubuhi saa 2, watu (wazungu kwa waswahili) wanakurupushwa kutoka maofisini na kwenda kujificha high-security area. Wazungu jasho linawatoka, waswahili meno nje. Kijana Prosper ameamua kuwafunza watu adabu.
Prosper ni mtaalamu wa mashine zote za kazi, kuanzia kubwa kabisa mpaka ndogo. Na wenzake walikuwa wanamuita "baba". Ndiye mtu wa kwanza kuendesha excavator lao kubwa kabisa pale North Mara, na kila mtu anatambua yeye ndio mtaalamu na mwalimu wao wa lile likitu. Na mtaalamu wa makitu mengine yote yanayotembea mule ndani.
Asubuhi hii, Prosper alikuwa juu ya loader lao kubwa kuliko yote, akilizungusha zungusha mbele ya maofisi yao. Kumbuka tairi la hii mashine linaipita urefu Land Cruiser; haya yanayovunja nyumba za watu huko tabata ni chamtoto kabisa. Prosper akawa ameshawaambia kwamba wampe hela yake, au atashusha na kusawazisha kila kilichosimama kwenye eno hilo. Na kila mtu alikuwa anajua hatanii, kwa sababu yeye ndio mtaalamu wa kutengeneza level-ground pale mgodini.
Wakati anafanya haya, production imesimama, kwa sababu loader hilo ndilo lililokuwa linatumika ku-feed mtambo wa kusaga mawe na kuzalisha dhahabu. Ni hasara kubwa tu huu mtambo usipofanya kazi hata kwa dakika kadhaa. Na prosper alikuwa anajua hili, na akawa anawaambia kwamba anajua wanaingia hasara kwa hiyo wampe hela yake haraka.
Na Prosper, jisni alivyomuungwana, alisisitiza kwamba hataki kingine chochote zaidi ya hela yake, aondoke. Na alifanya hivyo bila kumtusi mtu.
Sasa utapenda pale utaposikia kwenye redio koli Prosper akipewa taarifa kwamba dude lile lipo full-tank, kwa hiyo asiwe na wasiwasi hata siku mbili anaweza kukaa nalo. Utapenda zaidi pale utaposikia kwenye redio koli prosper akipewa taarifa kwamba FFU wamefika na wako maeneo gani. Utapenda zaidi na zaidi pale utaposikia Prosper akipewa taarifa kubadili njia kwa sababu FFU wanelekea anapoenda. Na utapenda zaidi na zaidi na zaidi pale utaposiki kwenye redio koli Prosper akiamuru hayo magari ya polisi yageuze la sivyo atafanya kitu mbaya, na yanageuza.
Naomba nisiielezee story nzima ingawa ni nzuri kama movie. Huwezi kuamini jinsi alivyokuwa anawapeleka-peleka wenye mgodi na wanausalama wa mgodi na wa serikali. Walijaribu kumkamata lakini wapi. Wakawa wanapanga wam-time akiliacha hilo dude wamkamate, lakini wapi. Yaani movie nzima ilipangwa na ikapangika.
Lakini mwisho wa siku, Prosper akawa amelipwa, summarily dismisal ikawa imefutwa akapewa barua aliyokuwa anataka yeye. Na ni jinsi gani amekabidhiwa bila kukamatwa, pia ni bonge la movie. Yaani utagundua dogo alikuwa sio kama wengi wetu. Na utazidi kubaki mdomo wazi ukijiuliza aliwezaje kulipata hilo dude asubuhi hiyo wakati yeye ashafukuzwa kazi na security kule ni ya hali juu.
Na kuanzia siku hiyo, wazungu, hasa mkuu wa mgodi, heshima tele. Kuna siku kijana mwingine alikwa anataka mafao yake, mkuu wa mgodi, ambaye zamani alikuwa na kiburi, na ambaye kumbuka alikuwa hana time ya kumsikiliza Prosper, alimshika mkono na kumpeleka mwenyewe kwa malipo haraka haraka.
Ingawa walikuwa wanawatishia wengine kwamba Prosper is on the run, na anatafutwa na polisi, Prosper hakuwahi kukamatwa. Ilisikika baadaye kwamba Polisi nao waliingiwa na ubinadamu baada ya kuona wazi kwamba kijana alikuwa anapigania haki yake, kwa hiyo juhudi za kumsaka Tanzania nzima zilikufa. Na hata kama zisingekufa, nadhani kijana angewapa tabu kidogo kumpata.
Nina-propose tutoe nishani ya ujasiri kwa Prosper maana aliweza kuitafuta na kuipata haki yake katika mazingira ambayo wengi hugwaya. Na pia aliweza kuwaekea mazingira mazuri wafanyakazi wenzake waliobaki baada ya yeye kuondoka