GE2025 Wananchi wenyewe wataamua Mgombea udiwani awajibu wanaodai hajafanya chochote

GE2025 Wananchi wenyewe wataamua Mgombea udiwani awajibu wanaodai hajafanya chochote

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mgombea Udiwani wa Kata ya Muleba Mjini, Muhaji Bushako, amejibu tuhuma za baadhi ya watu waliodai kwamba hajafanya lolote muhimu kwa maendeleo ya kata hiyo.

Akizungumza mbele ya mgeni rasmi, Mgombea Ubunge wa Buchosa Eric Shigongo, Bushako alisema kwamba alipoanza kazi yake kama diwani alikuta zikiwa zimejengwa takribani mita 300 tu za barabara za lami.

Chini ya uongozi wake, amesema kuwa kilomita 10 za barabara za lami zimejengwa, taa za barabarani zimewekwa, na huduma za afya pamoja na umeme zimeboreshwa.

Bushako amesisitiza kuwa mafanikio hayo ndiyo sababu wananchi walimuunga mkono katika uchaguzi uliopita, huku akiomba waendelee kumuamini ili aendeleze miradi ya maendeleo ya kata hiyo endapo atachaguliwa tena.


 
Back
Top Bottom