Wananchi zaidi 90 Wilayani Kilwa mkoani Lindi wamerudisha kadi za ACT-wazalendo na CCM na kujiunga na chama cha wananchi CUF

Wananchi zaidi 90 Wilayani Kilwa mkoani Lindi wamerudisha kadi za ACT-wazalendo na CCM na kujiunga na chama cha wananchi CUF

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
IMG_20200708_094136_377.jpg
#HABARI WANANCHI ZAIDI 90 WILAYANI KILWA MKOANI LINDI WAMERUDISHA KADI ZA ACT-WAZALENDO NA CCM NA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WANANCHI CUF

Mkurugenzi wa mafunzo na udhibiti CUF Taifa Mhe. Masoud Omar Mhina kutoka kushoto ndiye aliyepokea Kadi hizo na Kuwakabidhi kadi za Chama Cha Wananchi CUF.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa mkoani Lindi wana imani na Chama Cha CUF kwani wanaamini ndiyo mtetezi wao sahihi na sio vyama vingine.

#2020KILWATENA.
 
😂😂😂😂😂
Kwisha habari yenu, mnaenda kuwa kama TLP na matawi mengine ya CCM.
 
Kutokana na aina ya siasa mbadala kuwa ya level hii, ndio maana sisi wengine tunaamini kuwa pamoja na changamoto zote, bado CCM ni chama chenye uafadhali sana kilichowaacha wengine kwa mbali sana.
 
Nyie mnasubiria kujizika tu maana mlikubali kuchezewa na msaliti Lipumba sasa wananchi tumewasusa, kwaherini
 
Ccm na cuf ya Lipumba hakuna mwenye afadhali
Kutokana na aina ya siasa mbadala kuwa ya level hii, ndio maana sisi wengine tunaamini kuwa pamoja na changamoto zote, bado CCM ni chama chenye uafadhali sana kilichowaacha wengine kwa mbali sana.
 
Pamoja na kadi "kutanuliwa" ili angalau zikaribie 45 bado zimegoma! Mleta mada umetimiza wajibu wako wa kikatiba, hahahahah!
Naona kuna ya CCM moja na ACT zipo kama 10 hivi. Siasa ya bongo ya kipumbavu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Habari bila picha hainogi ila kwa picha hizi mkuu wanasema umenyea kambi
 
Ukiona unapokea Wageni wengi sana na kwa ghafla mno hasa katika Kipindi cha Kuelekea Uchaguzi Mkuu jua ya kwamba wengi wao ni Nyoka tu.
 
CCM na hawara yao CUF wajinga kweli kweli wanaachapisha kadi za vyama vingine kisha wanaita waandishi wa habari kuzipiga picha, hii ni punieto ya kisiasa.
 
View attachment 1500625#HABARI WANANCHI ZAIDI 90 WILAYANI KILWA MKOANI LINDI WAMERUDISHA KADI ZA ACT-WAZALENDO NA CCM NA KUJIUNGA NA CHAMA CHA WANANCHI CUF

Mkurugenzi wa mafunzo na udhibiti CUF Taifa Mhe. Masoud Omar Mhina kutoka kushoto ndiye aliyepokea Kadi hizo na Kuwakabidhi kadi za Chama Cha Wananchi CUF.

Aidha wananchi hao wamesema kuwa mkoani Lindi wana imani na Chama Cha CUF kwani wanaamini ndiyo mtetezi wao sahihi na sio vyama vingine.

#2020KILWATENA.
Hizo kadi mbona zote ni mpya?!!!!
 
Wananchi wapumbavu kama professor mpumbavu.

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Huwezi kulinganisha CUF na TLP hata siku moja.Pamoja na mpasuko uliitokea bado CUF ina nguvu kipimo chake uangalie itakuwa na wagombea Mbunge wangapi na TLP wangapi.
 
Kurudisha kadi haikuwahi kuwa ni kujitoa kwenye chama chochote, ni sanaa tu!! Je kuna uhakiki gani wa rejista ya chama unafanyika kuthibitisha kuwa aliyeirudisha amejitoa??

Kuirudisha bila kuondolewa kwenye rejista ni sawa na kupoteza kadi na kutotoa taarifa kuwa hunayo tena!! Wengi wamelipia kadi zao miaka hata 20 mbele - kadi zao bado ni hai!!

Kuna mambo mengi sana hatujafika popote!!!
 
Back
Top Bottom