Wananchi zaidi ya 500 jimbo la Ziwa na Wawi visiwani Pemba warudisha kadi za ACT-Wazalendo wakabidhiwa kadi za CUF na Prof. Lipumba

CUF Habari

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2019
Posts
239
Reaction score
234
Screenshot_20200609-155733.png

Zaidi ya wananchi 500 wa Jimbo la Ziwani na Wawi visiwani Pemba wamerejesha kadi za Chama cha ACT Wazalendo mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na kusema kuwa wao ni wafuasi wa CUF kwa miaka zaidi ya 27 na si wafuasi wa ACT Wazalendo.

Pia wananchi hao wamemlilia Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kufuatia ubovu mkubwa wa barabara unaowakabili kwa kipindi kirefu sasa na kuomba pindi watakapowapa ridhaa ya kuingia kwenye Serikali ya kitaifa waweze kuwatatulia kero hiyo.

Wananchi hao wametoa kilio hicho wakati Mwenyekiti huyo wa CUF alipokuwa akizindua moja ya tawi la Bilikau kwenye ziara yake ya kichama visiwani humo.

Seleman Jumaa ni mmoja wa wananchi hao ambaye amesema, kila wanaposikia nyimbo za chama cha CUF nafsi zimekuwa zikiwauma sana na kujiona kwa nini watumikie ACT, chama ambacho hakijawatoa mbali.

”Mheshimiwa Mwenyekiti Lipumba mimi binafsi niliposikia hii nyimbo tu ya CUF imenikumbusha mbali sana na kujiona mkosaji kuhama CUF, leo hii nakukabidhi kadi hizi za wananchi wengi waliokwenda ACT wamesema wanataka kurudi nyumbani kwenye chama chao,”amesisitiza Jumaa.

Kwa upande wake mtia nia ubunge jimbo hilo, Mbaruk Seif Salum amesema, ameamua kugombea jimbo hilo kwa kuwa wabunge wengi waliopita si wakweli kwani wakipewa ridhaa wanawasahau wananchi.
 
Attachments

  • Screenshot_20200609-155733.png
    Screenshot_20200609-155733.png
    153.7 KB · Views: 2
Wanawadanganya hao. Yaani wamkatae mpemba mwenzao Seîf wamfuate mnyamwezi sijui msukuma IBRA
 
Pemba watu 500 ni sawa na jimbo la uchaguzi! lol
 
View attachment 1473247

Zaidi ya wananchi 500 wa Jimbo la Ziwani na Wawi visiwani Pemba wamerejesha kadi za Chama cha ACT Wazalendo mbele ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na kusema kuwa wao ni wafuasi wa CUF kwa miaka zaidi ya 27 na si wafuasi wa ACT Wazalendo.

Pia wananchi hao wamemlilia Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kufuatia ubovu mkubwa wa barabara unaowakabili kwa kipindi kirefu sasa na kuomba pindi watakapowapa ridhaa ya kuingia kwenye Serikali ya kitaifa waweze kuwatatulia kero hiyo.

Wananchi hao wametoa kilio hicho wakati Mwenyekiti huyo wa CUF alipokuwa akizindua moja ya tawi la Bilikau kwenye ziara yake ya kichama visiwani humo.

Seleman Jumaa ni mmoja wa wananchi hao ambaye amesema, kila wanaposikia nyimbo za chama cha CUF nafsi zimekuwa zikiwauma sana na kujiona kwa nini watumikie ACT, chama ambacho hakijawatoa mbali.

”Mheshimiwa Mwenyekiti Lipumba mimi binafsi niliposikia hii nyimbo tu ya CUF imenikumbusha mbali sana na kujiona mkosaji kuhama CUF, leo hii nakukabidhi kadi hizi za wananchi wengi waliokwenda ACT wamesema wanataka kurudi nyumbani kwenye chama chao,”amesisitiza Jumaa.

Kwa upande wake mtia nia ubunge jimbo hilo, Mbaruk Seif Salum amesema, ameamua kugombea jimbo hilo kwa kuwa wabunge wengi waliopita si wakweli kwani wakipewa ridhaa wanawasahau wananchi.
Ukisikia vichaa wanasema "Zaidi ya ......."

Ujue wanadanganya pakubwa...

Poropesa mavi
 
Endeleen kudanganyana,hlo tawi la chama chakavu limeshatumbukia choon
 
Duuuh cku hz ukisikia wamehama watu 500 jua ni watu 7 tu..cjui inawasaidia nn kuongea uongo..hvyo hvyo hata Nccr Mageuzi..walipokea wanachama 25 lkn wakaandika wamepokea wanachama 90,000 kutoka chadema wkt jimbo zima linawakazi 85600... daaah punguzeni uongo bc
 
lipumba profesa aliefilisika kifikra. kwanza ameoa?
 
Ni wa pemba wale ninao wajua mimi au wengine ambao kipindi kile hurudisha kadi za cuf na kujiunga ccm lakini kwenye kura humpa seif
 
Back
Top Bottom