PreGE2025 Wananchi zaidi ya elfu 10 wa Itezi waondokana na shida ya maji Mbeya

PreGE2025 Wananchi zaidi ya elfu 10 wa Itezi waondokana na shida ya maji Mbeya

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wananchi zaidi elfu 10,000 wa kata ya Itezi jijini Mbeya, wameondokana na shida ya upatikanaji wa maji safi baada ya Mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mbeya MBEYAUWSA, kuzindua mradi wa maji wa kisima kirefu kwenye shule za msingi Gombe na Mwasote jijini humo.

Eng. Barnabas Konga ni kaimu mkurugemzi wa mamlaka hiyo anasema utekelezaji wa mradi huo ni jitihada za kukabiliana na shida ya maji kwa jiji la Mbeya ambapo mamlaka tayari imechimba visima vitatu na ina mpango wa kuchimba visima vingine vitano, wakati wakisubiri kukamilika mradi mkubwa wa maji wa chanzo cha mto kiwira utakao kuja kumaliza shida ya maji.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizindua mradi huo wa kisima kirefu wenye uwezo wa kuzalisha maji lita laki tano kwa siku ulio ghalimu zaidi ya millioni 100, Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Mhe DorMohamed Issa amewaomba wananchi kuulinda na kutanza miundombinu ya mradi huo, huku Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi (MBEYAUWSA) Bi. Edna Mwaigomole akielezea manufaa ya mradi huo.
 
Back
Top Bottom