Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Nimekutana na mjadala huu mahali.Katika mjadala huo mjadala ulikuwa,je baada ya kufunga ndoa ni wakati gani ulikua unapata usingizi mzuri usiku? . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Je kabla ya ndoa au baada?Na ikatokea ukaulizwa je baada ya ndoa unataka uwe unalala kitanda tofauti au kimoja na mke/mume?(Ila kama ni tofauti utakapo hitaji haki ya ndoa unaweza kumfuata mwenzio kisha ukarudi kitandani kwako)Kutokana na majibu yalivyotolewa ilionekana umri ulichangia kuamua misimamo ya wachangiaji. . . . . . . . . . . . . . . . . . , . . . . . . . . . . . . . . . . . . .Wale walioonekana vijana zaidi(ndoa zisizokuwa na muda mrefu)walionekana kuufurahia na kudai wanapata usingizi mzuri zaidi baada ya ndoa na wasingependa kutengana na wenzi wao kitanda.Mambo yalikua tofauti kwa watu wazima,wao walionekana kupenda utengano wakati kulala. . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . . Sijajua ni kwanini umri umeonekana kigezo,labda kuna kuchokana au mvuto kuwa juu sijui.Vijana na wazee wa JF mlio kwenye ndoa maoni yenu yako vipi?