Wanandoa wapigwa risasi na kufa nchini Cameroon

Wanandoa wapigwa risasi na kufa nchini Cameroon

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Watu wasiojulikana na waliojihami kwa silaha katika mji mkubwa zaidi wa watu wanaozungumza Kiingereza nchini Cameroon, wamewaua takriban watu tisa, wakiwemo wanandoa wapya.

Simplice Lontsi Tsomene, 37, na Hélène Raisa Tanga, 25, walikuwa wazazi wa watoto watatu na walikuwa na duka la simu.

Waasi wanaopigania kujitenga wamelaumiwa kuhusika na shambulio hilo. Watu hao wenye silaha walifika kwenye makutano ya magari mawili ambayo hayakuwa na alama, huku wakiwapigia kelele watu walale chini, lakini wakaanza kufyatua risasi wakati baadhi ya wakazi waliokuwa na hofu walipojaribu kukimbia.

Walioshuhudia wanasema watu wenye silaha walishutumu waathiriwa kwa kuwa "miguu myeusi", wakipendekeza kuwa walikuwa wakishirikiana na serikali au hawakuheshimu maagizo ya wanaotaka kujitenga.

Waasi ambao wanataka kuunda nchi tofauti iitwayo Ambazonia kwa maeneo yanayozungumza Kiingereza ya Cameroon wamekuwa kwenye mzozo na serikali tangu 2017, na Bamenda ni moja wapo ya maeneo yao yenye nguvu.

Siku moja kabla ya mashambulizi haya ya hivi punde, wanajeshi walishambulia makazi katika mtaa huo wa Nacho, na kuua vijana watano.

Hali inazidi kuwa mbaya, huku ukiukwaji wa kutisha wa haki za binadamu na ukatili ukifanywa. Amnesty International hivi majuzi ilichapisha ripoti inayoelezea madai ya mauaji na ubakaji uliofanywa na pande zote mbili katika mzozo wa kivita wa Eneo linalozungumza Kiingereza na kuitaka serikali kufanya uchunguzi.

Ingawa hakuna kundi lililodai kuhusika na mauaji hayo, baadhi ya viongozi wa Ambazonia walioko ughaibuni wamekuwa wakiwataka wapiganaji wao kuwafuata wale wanaowaita "miguu myeusi", bila huruma.

CHANZO: BBC
 
... Cameroon once upon a time was a among the most peaceful countries in Africa including Cote de Ivoire! Hakuna mkataba wa ovyo kama huu muungano; alisikika the second in power pande zile akihamasisha.
 
Back
Top Bottom