Wanao jua uwezo na wema wako hawakutaji na wasio jua ndio hukutaja

Wanao jua uwezo na wema wako hawakutaji na wasio jua ndio hukutaja

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
Hivi umewahi kugundua kuwa kuna wengi ambao wanajua UWEZO na WEMA wako ila hawakutaji kabisaaaa!!!.

Ila kuna wachache ambao wanajua baadhi ya MADHAIFU yako na MABAYA yako na wanabidii sana ya kuyazungumzia.

Matokeo yake ni kuwa, mabaya yako yanasikika zaidi kuliko mema yako.

Halafu kibaya zaidi ni kuwa, wale ambao wanakujua vizuri HAWAKUELEZEI VIZURI.

Na wale ambao hawakujui ndio wana bidii ya kueleza yasiyo ya kweli.

Hivi unajua kuna fursa nyingi umezikosa kwa sababu kuna mtu alikaa kimya na alikuwa kwenye nafasi ya kukutaja na kukusemea vizuri.

Hivi unajua kuna watu wanakuchukia kwa sababu kuna mtu alikusema vibaya tena kwa kitu kisicho cha kweli?

Yale ambayo tunatamani kufanyiwa, nasi tuanze kwa kuwafanyia wengine.

Hebu leo mtaje kwa jina mtu mmoja

(Hebu Mtag) na elezea angalau sifa yake moja nzuri unayoifahamu.

Panda mbegu ya KUTAJA Leo ili nawe UTAJWE kesho.
 
Back
Top Bottom