Du kuna jirani yangu alinunua kifaa hiki tena kwa laki tatu, mwaka jana alikuta kinashika moto yaani ni Mungu tu ilikuwa weekend alikuwa nyumbani la sivo tungempa hifadhi Mabwepande
Japo sisi hatujawahi kupata tatizo kama hilo ndio maana Kifaa hiki zaidi ya kuwa na overload protection kina temperature protection hiyo yote ni kulinda mambo kama hayo.
Unajua mara nyingi vifaa vya umeme vinaungua kutokana na kukiuka maelekezo ya utumiaji;si hivi tu hata stabilizer nyingi zinaungua moto sababu unakuta kitu cha Watt 1000 mtu anafunga mzigo wa watt 2000,ingekuwa kwa kila mtu kinaungua ingekuwa tatizo la production.
Hata hivyo sisi tulilitambua hilo ndio maana kifaa hicho unacho kiona hapo juu kimewekewa protection za kulinda matumizi yasio takiwa kama ikitokea mteja akazidisha mzigo basi booster itajizima.
Na kitu kingene watu wamekuwa wakinunua stabilizer na kuzitumia kama booster kwenye visima vya maji ,hivyo husababisha zikaungua kwani stabilizer hazijatengenezwa kwa kazi kama hiyo!
Vifaa hivi ni salama,kuna watu kama 37 wamefungiwa na wanaendelea vizuri na wengine guarantee zao zimeisha siku zote hakikisha unafata maelekezo ya matumizi!
Na kuna watu wengine wanazitengeneza hizi bila kuweka security system wanatumia step-up transformer basi hii pia ni sababu ya kiufundi inayoweza kusababisha kifaa kama hiki kuungua!
Kuna mwingine alinunua dukani stabiliza ya watt 5000 ikaja ikaungua sababu tu aliitumia kama booster wakati ile ni stabilizer. Kiutaalamu stabilizer haitakiwi kutumika eneo ambalo lina umeme chini ya volt 110.