Wanaobeba vifurushi mgongoni huku wakiomba barabarani huwa wanabeba nini?

Wanabeba ID zao
 
Nimecheka kweli kweli. Nadhani hakuna haja ya kuogopa kwa sababu hawezi kukufanya chochote. Japokuwa inawezekana kabisa alikuwa na nia ovu au alitumwa na mganga kufanya hivyo, lakini kwangu mimi huwa naona watu wa aina hiyo wanapoteza muda tu. Mbaya ni ikiwa utalishwa kitu kwani inaweza kuwa sumu au uchafu mbaya sana. Babu yangu ambaye ni marehemu sasa, kijijini huko, kuna siku alikuwa anatembea njiani, wakati nikiwa mdogo kama miaka 17 hivi, nikaona jirani yetu, mwanamke akamlia timing, na kwenda kuzoa mchanga wa sehemu aliyokanyaga, yaani unyayo ulipokanyaga. Nikaja kumwambia, akacheka kweli kweli na kusema achana naye huyo, mwache azoe mpaka ajaze lori.
 
Kuna Mchaga alienda dodoma akawakusanya wenye ukoma akawaketa dar akawachukulia nyumba mzima kule kiwalani.Basi aliwanunulia wheelchair kila mmoja halafu kila mtu kamuwekea muhasibu Kwa maana yule anayemsukuma,Kila jioni wanaleta hesabu ukizingua unapakizwa ndani ya gari unarudishwa Dom.Mchaga yule anatengeza pesa hatari.
 
Duh!...maji na pesa ni coincidence tu......

ungempa pesa na mauzo yakawa mabaya ungesema pia ni chuma ulete.
 
Wanabebeaga ballistic missile zakutungulia wanyima omba omba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…