KERO Wanaochimba mchanga Bunju Dogodogo Centre wanahatarisha maisha ya nyumba zetu, NEMC hawasaidii chochote

KERO Wanaochimba mchanga Bunju Dogodogo Centre wanahatarisha maisha ya nyumba zetu, NEMC hawasaidii chochote

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni mkazi wa Bunju Dogodogo Centre, kero yangu ni malori ya mchanga kuchimba mchanga bondeni karibu na makazi ya watu.

Hali hiyo imekuwa ikihatarisha nyumba za Wakazi kubomoka kwa kupitiwa na bonde linaloendelea kujitokeza.

Serikali ya Mtaa imejaribu kila njia lakini bila mafanikio, imekuwa kama vile ni halali kuchimba mchanga hili eneo ili hali kuna mabango ya NEMC kukataza, baadhi ya Maafisa wa Mazingira wakishirikiana na Polisi wanakuja kuchukua rushwa waziwazi.

Tusaidiwe kwa kuwa maeneo yetu yanazidi kuharibika na tupo hatarini.
photo_2026-02-11_08-18-22.jpg

photo_2026-02-11_08-18-25.jpg

photo_2026-02-11_08-18-27.jpg

photo_2026-02-11_08-18-28.jpg
 
Mito yote sasa hivi ni vurugu mechi MTO msimbazi maeneo ya kuelekea kinyerezi ni kuchota mchanga kama hawana akili nzuri sijui NEMC inafanya nini
 
Back
Top Bottom