Mimi ni mkazi wa Bunju Dogodogo Centre, kero yangu ni malori ya mchanga kuchimba mchanga bondeni karibu na makazi ya watu.
Hali hiyo imekuwa ikihatarisha nyumba za Wakazi kubomoka kwa kupitiwa na bonde linaloendelea kujitokeza.
Serikali ya Mtaa imejaribu kila njia lakini bila mafanikio, imekuwa kama vile ni halali kuchimba mchanga hili eneo ili hali kuna mabango ya NEMC kukataza, baadhi ya Maafisa wa Mazingira wakishirikiana na Polisi wanakuja kuchukua rushwa waziwazi.
Tusaidiwe kwa kuwa maeneo yetu yanazidi kuharibika na tupo hatarini.