Nelson...
Umepotea na darsa lako.
Wakati tunakusubiri nimeona nijaze ombwe hili kwa mimi kutoa darsa kwako na kwa wanafunzi wangu ambao niliwaambia kuwa utatoa darsa na nimewaalika wafuatilie utusomeshe sote.
Kumekuwa na vichekesho kidogo nilipowaambia kuwa wewe umekusudia kunisomesha mimi.
Lakini haya tuyaache kwa sasa.
Naweka hapo chini darsa langu:
''Wazanzibari na Miaka 25 ya Sanduku la Kura Faida Ipi Imepatikana?''
Historia ya chaguzi za Zanzibar kuanzia mwaka wa 1995 hadi 2020 imegubikwa na umwagikaji damu.
Hii mosi.
Pili ambacho kimekuwa kama sehemu ya kudumu ya chaguzi hizi ni kwa ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) kushindwa kutoa matokeo kwa wakati ingawa kura zinaweza zote zikahesabiwa kwa siku moja.
Tatu ni udanganyifu.
Nne ni kutangazwa matokeo ya kura ambayo yana shaka.
Hili limekuwa sehemu ya uchaguzi Zanzibar.
Lakini katika haya yote tukio lililotia fora ni katika uchaguzi wa 2015 pale uchaguzi wote ulipofutwa na kuitishwa upya.
Haya yalifuatia uchaguzi wa 2010 ambao ofisi za ZEC zilizingirwa na wapigaji kura wakidai watoe matokeo.
ZEC haikuwa katika hali ya kuweza kutoa matokea.
Katika uchaguzi wa marudio 2015 uchaguzi ukawa ni kichekesho kwani hapakuwa na uchaguzi ingawa ZEC iliona imefanya uchaguzi.
Baada ya kupitishwa kwa kuwapo kwa SUK wapiga kura wa Zanzibar waliamini kuwa pakiwa na SUK Zanzibar itatulia na uchaguzi hautosababisha kumwagika kwa damu ya mpiga kura yeyote wala kuvurugika kwa uchaguzi wenyewe.
Haya haya hayakuwa.
Uchaguzi wa 2020 kama chaguzi tano zilizopita nao ukawa na matatizo kiasi wafuatiliaji wengi wa siasa za Zanzibar wakaamini kuwa CCM Zanzibar imeshindikana.
CCM Zanzibar haiko tayari kwa chaguzi huru na haki.
CCM Zanzibar ina hofu kubwa ya sanduku la kura.
Inaamini kuwa haina uwezo wa kushinda uchaguzi huru na wa haki.
Lakini nini sababu ya CCM Zanzibar kuliogopa sanduku la kura?
Sababu ni uchaguzi wa kwanza wa mwaka wa 1995 Salmin Amour aliposhindwa na Maalim Seif.
Ilikuwaje CCM chama kilichokuwa madarakani kishindwe na CUF chama kichanga?
Matokeo ya uchaguzi ule uliwadhihirishia viongozi wa CCM Zanzibar Wazanzibar hawawataki na ndiyo sababu ya kuwanyima kura.
Hii maana yake ni kuwa Wazanzibar hawayathamini mapinduzi.
Mapinduzi hayawezi tena kuwa daima.
Mapinduzi yamefikia kikomo sasa yako ukingoni.
Matokeo yake ikawa CCM kila uchaguzi inachukua serikali kwa mabavu kwa msaada kutoka Tanganyika.
Ikawa kila uchaguzi Wazanzibari wanauawa.
Katika hali hii kikawa kimeingia kitu kipya katika kuchagua viongozi Zanzibar.
Kitu hiki kipya Wazanzibari wanakiita ‘’Usultani Mpya.’’
Watoto wa marais wakawa sasa wanagombea nafasi za Urais.
Alianza Amani Karume akafuatia Dr. Hussein Mwinyi.
Bahati mbaya watoto wa marais waliopita wamegombea nafasi za baba zao lakini hawakushinda na damu ya wapiga kura Wazanzibari ikamwagika.
Katika uchaguzi wa 2020 ACT Wazalendo walikubali kuingia katika SUK na kubwa lililokuwa likitafutwa ni kuwepo kwa amani visiwani.
Pawe na amani Zanzibar pasiwe na sababu ya kuendelezwa kwa kukamatwa watu kupigwa na wengine kufungwa jela na wengine kuuliwa kabisa.
Jambo kubwa lililojitokeza baada ya uchaguzi wa 2020 ni kusikika kwa lugha kutoka kwa Wazanzibari kuwa ni lazima SUK iridhiwe na ACT Wazalendo iiingie katika serikali ili damu ya Waislam isimwagike kwa sababu ya ukaidi wa wanasiasa.
Rais Hussein Mwinyi leo ni Rais wa Zanzibar.
Juu ya haya yote kuna jambo moja linalohangaisha vichwa vya viongozi wa CCM Zanzibar.
CCM Zanzibar ina uwezo wa kushinda uchaguzi huru na wa haki uchaguzi ujao 2025?
Hapa ndipo Zanzibar ilipo hivi sasa.