Nelson Jacob Kagame
JF-Expert Member
- Dec 26, 2022
- 9,576
- 13,545
- Thread starter
-
- #361
Darasa sio hapa kuna sehemu inaandaliwa na ninaalika pia wanazuoni wa kidini na wazee wa ASP na TANU na ACT Wazalendo na CUF!!!!Usiwe na haraka nimekwambia uwe radhi kufundishika usijali!!Ndugu zanguni,
Nelson tunamsubiri aingie darasani.
Wanafunzi tunamsubiri.
Mimi bado sijabanduka hapa toka Maghrib.
Bado nasubiri.
Kwakuwa umeyatakaSasa nakuuliza mimi wa mwanzo
Hivi sasa hakuna ubaguzi na haki ipo Zanzibar ?? na Tangnyika ??
Bwana Yesu alisema wengine huzaliwa si rizki .. Math 19:10-12Darasa sio hapa kuna sehemu inaandaliwa na ninaalika pia wanazuoni wa kidini na wazee wa ASP na TANU na ACT Wazalendo na CUF!!!!Usiwe na haraka nimekwambia uwe radhi kufundishika usijali!!
Darasa langu ni la uso kwa uso!!!Sio wanafunzi wangu wote wana access za social network,s mzee wangu!!!!Kuna sehemu naandaaNelson...
Huna haja ya kuhangaika nisomeshe hapa mtandaoni darsa linufaishe wanafunzi wengi.
Hizi ndiyo njia za kisasà.
Unaweza kutumia zoom au clubhouse.
Ukiona hayo mazito kwako somesha hapa hapa JF.
Kwakuwa umeyataka
Swali lako liko vague ila nipo tayari kulijibu lakini kwanza Fafanua ili lieleweke na tuwe na kitu specific
Una maanisha nini kusema ubaguzi?
Na ni ubaguzi wa nani dhidi ya nani?
Ubaguzi ktk siasa? Kilimo? Biashara? Jamii? Elimu? Mfumo wa haki? Mfumo
Wa uzalishaji mali?
Wanadai uliwakana wenzio hadharani kua huwajui!!Nelson...
Mimi niseme nini?
Kama nilihusika na hizo shutuma mbona sikukukamatwa na kufikishwa mahakamani nijitetee?
Mkuu nimekuomba ufafanue swali lako ili nikupe jibu specific pia inakuwa kazi kwakokama ulivyouuliza wewe kwa sultani huo ubaguzi haupo na hizo haki zipo hivi sasa Zanzibar na Tanganyika ??
Wanadai uliwakana wenzio hadharani kua huwajui!!
Sijapotea nimeshakupa utaratibu wa darasa litakua wapi!!!!Ngoja nikamilishe utaratibu!!!!Toka mwanzo nilikusihi uwe na subra na uwe radhi kufundishikaNelson...
Umepotea na darsa lako.
Wakati tunakusubiri nimeona nijaze ombwe hili kwa mimi kutoa darsa kwako na kwa wanafunzi wangu ambao niliwaambia kuwa utatoa darsa na nimewaalika wafuatilie utusomeshe sote.
Kumekuwa na vichekesho kidogo nilipowaambia kuwa wewe umekusudia kunisomesha mimi.
Lakini haya tuyaache kwa sasa.
Naweka hapo chini darsa langu:
''Wazanzibari na Miaka 25 ya Sanduku la Kura Faida Ipi Imepatikana?''
Historia ya chaguzi za Zanzibar kuanzia mwaka wa 1995 hadi 2020 imegubikwa na umwagikaji damu.
Hii mosi.
Pili ambacho kimekuwa kama sehemu ya kudumu ya chaguzi hizi ni kwa ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) kushindwa kutoa matokeo kwa wakati ingawa kura zinaweza zote zikahesabiwa kwa siku moja.
Tatu ni udanganyifu.
Nne ni kutangazwa matokeo ya kura ambayo yana shaka.
Hili limekuwa sehemu ya uchaguzi Zanzibar.
Lakini katika haya yote tukio lililotia fora ni katika uchaguzi wa 2015 pale uchaguzi wote ulipofutwa na kuitishwa upya.
Haya yalifuatia uchaguzi wa 2010 ambao ofisi za ZEC zilizingirwa na wapigaji kura wakidai watoe matokeo.
ZEC haikuwa katika hali ya kuweza kutoa matokea.
Katika uchaguzi wa marudio 2015 uchaguzi ukawa ni kichekesho kwani hapakuwa na uchaguzi ingawa ZEC iliona imefanya uchaguzi.
Baada ya kupitishwa kwa kuwapo kwa SUK wapiga kura wa Zanzibar waliamini kuwa pakiwa na SUK Zanzibar itatulia na uchaguzi hautosababisha kumwagika kwa damu ya mpiga kura yeyote wala kuvurugika kwa uchaguzi wenyewe.
Haya haya hayakuwa.
Uchaguzi wa 2020 kama chaguzi tano zilizopita nao ukawa na matatizo kiasi wafuatiliaji wengi wa siasa za Zanzibar wakaamini kuwa CCM Zanzibar imeshindikana.
CCM Zanzibar haiko tayari kwa chaguzi huru na haki.
CCM Zanzibar ina hofu kubwa ya sanduku la kura.
Inaamini kuwa haina uwezo wa kushinda uchaguzi huru na wa haki.
Lakini nini sababu ya CCM Zanzibar kuliogopa sanduku la kura?
Sababu ni uchaguzi wa kwanza wa mwaka wa 1995 Salmin Amour aliposhindwa na Maalim Seif.
Ilikuwaje CCM chama kilichokuwa madarakani kishindwe na CUF chama kichanga?
Matokeo ya uchaguzi ule uliwadhihirishia viongozi wa CCM Zanzibar Wazanzibar hawawataki na ndiyo sababu ya kuwanyima kura.
Hii maana yake ni kuwa Wazanzibar hawayathamini mapinduzi.
Mapinduzi hayawezi tena kuwa daima.
Mapinduzi yamefikia kikomo sasa yako ukingoni.
Matokeo yake ikawa CCM kila uchaguzi inachukua serikali kwa mabavu kwa msaada kutoka Tanganyika.
Ikawa kila uchaguzi Wazanzibari wanauawa.
Katika hali hii kikawa kimeingia kitu kipya katika kuchagua viongozi Zanzibar.
Kitu hiki kipya Wazanzibari wanakiita ‘’Usultani Mpya.’’
Watoto wa marais wakawa sasa wanagombea nafasi za Urais.
Alianza Amani Karume akafuatia Dr. Hussein Mwinyi.
Bahati mbaya watoto wa marais waliopita wamegombea nafasi za baba zao lakini hawakushinda na damu ya wapiga kura Wazanzibari ikamwagika.
Katika uchaguzi wa 2020 ACT Wazalendo walikubali kuingia katika SUK na kubwa lililokuwa likitafutwa ni kuwepo kwa amani visiwani.
Pawe na amani Zanzibar pasiwe na sababu ya kuendelezwa kwa kukamatwa watu kupigwa na wengine kufungwa jela na wengine kuuliwa kabisa.
Jambo kubwa lililojitokeza baada ya uchaguzi wa 2020 ni kusikika kwa lugha kutoka kwa Wazanzibari kuwa ni lazima SUK iridhiwe na ACT Wazalendo iiingie katika serikali ili damu ya Waislam isimwagike kwa sababu ya ukaidi wa wanasiasa.
Rais Hussein Mwinyi leo ni Rais wa Zanzibar.
Juu ya haya yote kuna jambo moja linalohangaisha vichwa vya viongozi wa CCM Zanzibar.
CCM Zanzibar ina uwezo wa kushinda uchaguzi huru na wa haki uchaguzi ujao 2025?
Hapa ndipo Zanzibar ilipo hivi sasa.
Yani hata kuToa hata maana ya Ubaguzi huwezi?kama ulivyouuliza wewe kwa sultani huo ubaguzi haupo na hizo haki zipo hivi sasa Zanzibar na Tanganyika ??
Mkuu nimekuomba ufafanue swali lako ili nikupe jibu specific pia inakuwa kazi kwako
Nimekuwekea na options ili usipate tabu wewe uchague tu pia huwezi
Ndio maana nina mashaka na elimu yako
Nakupa nafasi nyingine twende kisomi
Fafanua swali ili tuwe na kitu specific mkuu nikujibu ipasavyo
Huyu jamaa niliacha kumjibu baada ya kugundua elimu yake ndogo sana katika siasa na historia!!!Mkuu nimekuomba ufafanue swali lako ili nikupe jibu specific pia inakuwa kazi kwako
Nimekuwekea na options ili usipate tabu wewe uchague tu pia huwezi
Ndio maana nina mashaka na elimu yako
Nakupa nafasi nyingine twende kisomi
Fafanua swali ili tuwe na kitu specific mkuu nikujibu ipasavyo
Yani hata kuToa hata maana ya Ubaguzi huwezi?
Kama huwezi hivi utakuwa unajua unachokiongelea kweli?
Una elimu gani ?
Ndiyo niliuliza mambo specific kuhusu umiliki ardhi, umiliki wa nyenzo za uzalishaji mali, umiliki wa watumwa n.kkwani ulipoweka hizo shutuma zako ulifafanua ??
Mbona unamlaumu sheikh Mohammed na wewe unafanya hayohayo , au ndio nyani haoni makalio yake
Huyu jamaa niliacha kumjibu baada ya kugundua elimu yake ndogo sana katika siasa na historia!!!
WatajeWapo wengi tu!!!!Sijui ajenda zao ni zipi nyuma ya pazia!!!
Ni kweli ni wazi hajui vingiHuyu jamaa niliacha kumjibu baada ya kugundua elimu yake ndogo sana katika siasa na historia!!!
Mzee Said Mohamedi na wengineoWataje
Rejea post no #279kwani ulipoweka hizo shutuma zako ulifafanua ??
Mbona unamlaumu sheikh Mohammed na wewe unafanya hayohayo , au ndio nyani haoni makalio yake
Ukimpa swali anakwepa sasa huo sio maana ya mdahalo wa kisomi!!!Mm nilimpuuzia kakaNi kweli ni wazi hajui vingi