Sultan MackJoe Khalifa
JF-Expert Member
- Nov 24, 2022
- 6,782
- 14,148
Hayo mapinduzi ndo yamezaa chama cha mapinduzi.shida tupu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sultan...Hayo mapinduzi ndo yamezaa chama cha mapinduzi.shida tupu.
Sasa mzee wangu wengine wakitoa maoni hujisikii vizuri why?????Afu usijikweze sana mzee wangu kuhusu CV yako maana siijui labda uniletee hapa niione itakua jambo la kheriNelson...
Nimesoma Ancient History.
Hii ni nyuma sana ya hapo.
Wakati mwingine hunyamaza kwa kukuonea huruma.
Nimehisi ulivyotaabika kusoma CV yangu.
Sikujisikia vizuri kukuonyesha kuwa ujiangalie.
Nisaidie ili tutunze heshima zetu.
Msomi haogopi kuhojiwa mzee wanguGavana...
Hawa hawana chochote kaka ni kibri tu.
Huyu kweli ndiye wa kunihoji mimi historia ya Karume?
Sasa uzi wangu kuhusu mapinduzi matukufu ya zanzbar mumegeuza uwanja wa kidini???????Hizbu hamna hoja zaidi ya udini???Gavana,
Nakuwekea picha ya moja ya misikiti iliyoko Cardiff, Wales.
Huu msikiti unaitwa ''Dar-ul- Isra.''
Huu ndiyo ulikuwa msikiti wangu.
Wahindi wa Pakistan walinunua kanisa wakaligeuza kuwa msikiti.
Wakanunua kanisa lingine jirani na hili lakini niliporudi Cardiff mwaka wa 1993 nikakuta bado liko vilevile hawajaligeuza kuwa mskikiti ila wanalitumia kama store ya kuwekea vitu.
View attachment 2507502
majibu mazuri na yenye hekima, ni moyo wa mtu tu uamue kubaki na misimamo kwasababu ya husda na chuki.Sultan...
Niruhusu nizungumze na wewe kuhusu shida lakini kwa kitu kingine baadae nitakujibu In Shaa Allah kuhusu mapinduzi.
Kuna mtu kaniuliza kwa nini simjibu mtu fulani (kataja identify yake) ilhali yeye akimsoma na akinitazama mimi hana makamo yoyote.
Nikamwambia nimemjibu, "Ahsante."
Akaniambia hilo si jibu umemshukuru.
Nikamwambia naam nimemshukuru na hiyo shukurani yangu kwake ndiyo jibu langu.
Nikamwambia kuwa ningemjibu kwa kumjibu maneno yake ningemuongezea ghadhabu na hili ni vizuri kuliepuka.
Huyu ndugu yetu moyo wake umejaa hasad na husda ni sumu inayokula kiwiliwili na ni kitu hatari.
Nikamwambia huyu ndugu yangu tupitie pamoja yote aliyoniandikia nami nikakaamua kuwa kimya na nikamshukuru.
Tukafanya hivyo.
Nikamuuliza nini alichokiona.
Jibu alilonipa kasema hakika huyu ni hasid.
Nikamuuliza kwa nini unamwita hivyo akasema, "Yote uliyotueleza na kutuonyesha kwa nia nzuri tuelewe na jibu ulilompa la kuwa si kila kitu unaweza kupata yakini yake ijaza yake ni kukutolea fedhuli?
Mbona yeye hatuwekei aliyofanya katika medani ya usomi?"
Sasa nikamjibu huyu ndugu yangu kuwa na hasad ndani ya moyo wake imefunika yote ambayo kwayo mimi yameniweka juu kileleni.
Husda yake inamuonyesha kile kitu kidogo kisichokuwa na maana yoyote.
Akaona ijaza yangu ni hayo maneno ya kejeli kwa sababu kaumizwa na kile ambacho yeye hana Allah bado hajampa.
Husda inamfanya aamini kuwa yeye hawezi kupata nilichopewa mie.
Kama kawaida ya mahasidi
wote hakuweza kustahamili akakitapika kile kinachomchoma - kuhadhiri kwangu Vyuo Vikuu, Afrika, Ulaya na Marekani na mengineyo.
Kuandika vitabu na kuchapwa na wachapaji wa sifa duniani.
Si kila mwandishi kazi yake inachapwa na Oxford University Press.
Si kila kitabu kinapewa nafasi ndani ya Cambridge Journal of African History.
Walimu wangu walionisomesha mimi hawajaingia ndani ya majarida ya kimataifa.
Anasema yeye haya kuwanayo mimi hayamshughulishi.
Lakini ukweli ni kuwa yote anayoyaona kwangu kwa ushahidi wenye ithibati yanamchoma.
Kashindwa kustahamili.
Alikuwa kimya lakini kapata upenyo kaona autumie kutema nyongo yake.
Vitabu vyote na "paper" zote nilizoweka hapa basi ziwe si lolote kwa kumdokolea tafiti moja tu ya kimya?
Turudi kwenye mapinduzi.
Zanzibar imetulia na In Shaa Allah itavuka huu mtihani.
Wazanzibari wamekubaliana kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK).
Agenda ya Wazanzibari ni kukubaliana kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Hawako mbali kufikia lengo hili.
(Ndugu yangu uliyeniomba nitoe jibu nimefanya kama ulivyosisitiza nifanye).
Nelson...Uzi wangu unazungumzia mapinduzi matukufu ya zanzbar!!!Msiubadilishe kua wa mambo ya dini!!!Sisi ASP na TANU hatunaga mambo ya udini!!!!Karibuni sana tuendelee
Sultan...majibu mazuri na yenye hekima, ni moyo wa mtu tu uamue kubaki na misimamo kwasababu ya husda na chuki.
Nelson...Msomi haogopi kuhojiwa mzee wangu
Nelson...Sasa mzee wangu wengine wakitoa maoni hujisikii vizuri why?????Afu usijikweze sana mzee wangu kuhusu CV yako maana siijui labda uniletee hapa niione itakua jambo la kheri
Tatizo ni moja mzee wangu unajikweza sana na muoga wa maoni kinzani!!!Huukubali ukweli unaopingana na maoni na mapokeo yako ya kisiasa na kidini sasa wasomi hawapo hivyo!!!!Huo ndio udhaifu wako mzee wanguNelson...
Nitakuambia kitu.
Kwanza mimi sithubutu kujikweza kwani si katika mafunzo yetu Wswahili.
Ila nitajinasibu kwako kuondoa kejeli na dharau unayoonyesha kwangu.
Kuna mtu katika mjadala uliovunja rekodi JF ulioanzishwa na Yeriko Nyerere kiasi cha miaka 10 iliyopita kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mjadala ulidumu kwa miezi sita mfulululizo na kupitiwa na takriban watu 1 m.
Haikupata kutokea hadi leo.
Kila jibu nililotoa katika historia ya uhuru kwa wengi jibu lilibeba historia ambayo haikuwa inafahamika popote.
Kuna msomaji mmoja akashindwa kustahamili akawaambia wenzake kuwa kila wanaponiuliza maswali ndipo ninapoeleza mengi ynayoumiza.
Mimi napenda sana kuulizwa maswali kwani nafaidika na maswali.
Kama si JF mimi nisingejulikana kwa wengi.
Siku Maxence Melo alipokuja nyumbani kwangu kunipa cheti changu na zawadi ya simu kwa ajili ya uandishi wa historia hapa JF nilimshukuru na kumwambia kuwa kama si yeye nani angenijua mimi?
JF imechapa kila kitui nilichoandika hawakupata kukataa hata makala yangu moja.
JAMII FORUMS NA MAKALA ZA MOHAMED SAID:UKIPENDA KUSOMA HISTORIA YA TANGANYIKA/TANZANIA
''HISTORIA YA UHURU ISIMULIWAVYO NA MOHAMMED SAID YAKOSOLEWA''
Mjadala huo hapo juu katika Jamii Forums ulivunja rekodi kwa kuwa ulidumu kwa miezi sita mfulululizo na ulichangiwa na watu zaidi ya 900,000.
Aliyefungua uzi huu alifanya hivi baada ya kusoma makala zangu za historia ya uhuru wa Tanganyika nikieleza mchango makhsusi uliotolewa na Waislam wa Tanganyika ambazo kwa kweli kwa wengi historia hii ilikuwa mpya kwao.
Katika Makala zangu niliweka picha ambazo ambazo wengi hawakupata kuziona kabla na walisoma mengi ambayo walikuwa hawajapata kusoma wala kusikia kabla.
Wengi waliingia kuchangia kwa kutaka kutafuta ukweli na wako wengi walioingia wameghadhibika wakimuona mwandishi kama ‘’mchochezi’’ na Muislama wa ‘’Siasa Kali.’’
Wako wachache waliingia kuchangia kwa kuniunga mkono na kunipongeza kwa kuandika historia ambayo ilikuwa imepotezwa kwa miaka mingi.
Haya yalitokea sasa imepita karibu miaka 10.
Nina wajibu wa kuishukuru JF kwani wao walichapa kila makala niliyoandika.
JF kwa kufanya hivi ikanijengea jina na watu wengi wakanijua na watu wengi sana wakatambua kuwa kwa miaka mingi sana walikuwa wanasoma historia ya uhuru ambayo ilikuw ana upungufu mkubwa usiolelezeka.
Kwa mchango wangu huu JF wakanitunuku Cheti cha Shukurani na kunizawadia Simu Janja.
Mambo yalikuwa kama hivi:
''...leo hii umesomwa na watu 490, 472 na unaendelea kusomwa daah!!. Kuna huu uzi mwingine unamuhusu Mudeer Mohamed Said, huu ulianzishwa na Mag3 huu umeishasomwa na watu 112, 133 huu bado upo hewani unaweza kuupitia hapa chini kiduchu... Historia ya Uhuru isimuliwavyo na Mohammed Said yakosolewa...''
Hapa jamvini ndipo watu waliponifahamu na kuona kazi nilizoandika.
View attachment 2508371
Unaona mapungufu yako unadhani unajua kila kitu sababu ulizaliwa 1950 pale kariakoo!!Wasomi hatupo hivyo mzee wanguNelson...
Basi wewe ndiyo wa kunihoji mimi kwa historia usioijua?
Wewe unakuja kwangu kusoma siyo kuhoji.
Una chochote cha kuonyesha kuwa unajua unachohoji kwangu?
Mada ni mapinduzi ya zanzbar wewe ushaingiza udini!!!Sitaki kuamini una tatizo la kichwani mzee wanguSultan...
Ubaya wa husda ni kule kumtesa hasid kwa neema ambazo Allah kamjaalia mja wake.
Kila umuonapo mtu na kheri za Allah wewe unaumia na moyo kujawa chuki.
Nina uzoefu wa kutosha sana katika hili.
Okello hawamtambui ushawahi siku ya mapinduzi akitajwa popote? Sana sana atatajwa Karume ndio shujaa wa mapinduziKuna watu hapa afrika mashariki wanabeza sana mapinduzi ya Zanzibar yaliyoongozwa na Mh Okello na kufanya miadhara kuyaponda!!!Wana ajenda gani nyuma ya pazia?
Ana role yake inajulikana na karume ana role yake inajulikana!!!Wote ni mashujaa kwetuOkello hawamtambui ushawahi siku ya mapinduzi akitajwa popote? Sana sana atatajwa Karume ndio shujaa wa mapinduzi
Unaona sasa akili yako ni udini tu mzee wangu!!!!Sisi CCM hatupo hivyoNelson...
Uislam (unaogopa kutaja) ni sehemu muhimu sana ya ''political history'' ya Tanganyika kwa ajili ya yale ambayo walifanya katika kukabiliana na Wajerumani na Waingereza.
Kujaribu kukwepa ukweli huu hakuondoi ukweli huu.
Ilijaribiwa kufanywa hivyo lakini leo angalia balaa lake baada ya mimi kuandika historia ya Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Watu wanasoma upya historia ya uhuru.
Zanzibar ni nchi ya Waislam wengi ukipenda weka 99%.
Huwezi kuandika historia ya Zanzibar nje ya Uislam.
Nelson unajinadi na kujitangaza kuwa wewe ni ASP.
Huwezi kuwa ASP wala haihitaji ujuzi mkubwa kutambulika kuwa wewe unadanganya.
Mimi sijajinadi hivyo kwa historia ya mshikamano wa wazee wetu na ASP itakuwa wewe?
Niambie ni lini ulisikia akitajwa kua yeye ndie aliefanikisha mapinduzi, yaan namaanisha wananchi wa Zanzibar wakisifu kua Okello ni shujaa wao kawakomboa kutoka kwa Mwarabu? Sana sana wanaona mmewaharibia michongo yao tu wao wanajiona hawana tofauti na watu wa Oman na QatarAna role yake inajulikana na karume ana role yake inajulikana!!!Wote ni mashujaa kwetu
Umezaliwa enzi gani mdogo wangu???? 1960,s au 1970,s au 1980,s nijibu kwanza afu nitakujuza mdogo wanguNiambie ni lini ulisikia akitajwa kua yeye ndie aliefanikisha mapinduzi, yaan namaanisha wananchi wa Zanzibar wakisifu kua Okello ni shujaa wao kawakomboa kutoka kwa Mwarabu? Sana sana wanaona mmewaharibia michongo yao tu wao wanajiona hawana tofauti na watu wa Oman na Qatar
Karibu CCM upate darasa la uzalendo kwanza!!Niambie ni lini ulisikia akitajwa kua yeye ndie aliefanikisha mapinduzi, yaan namaanisha wananchi wa Zanzibar wakisifu kua Okello ni shujaa wao kawakomboa kutoka kwa Mwarabu? Sana sana wanaona mmewaharibia michongo yao tu wao wanajiona hawana tofauti na watu wa Oman na Qatar