Uchaguzi 2020 Wanaodhani ACT-Wazalendo na CHADEMA kushindwa kusimamisha mgombea mmoja ni uchu wa madaraka mnakosea, ni mbinu sahihi kuwabana NEC na CCM

Mbona mnahisi kuna uwezekano wa mmoja kuenguliwa, mna hofu na sifa zake!!
 
Mwanahabari Huru Salary Slip mmeliona hili andiko? The obvious ni kuwa kuna watu wataenguliwa hasa CDM na ACT... tunafanyaje?
 
kwanini unasema hivyo? Mbona yeye mhusika kanijubu

Ni sawa kwa vile kaamua kukujibu, ni kwa ujasiri wake na amesema anajiamini. Ila mi niliona ni swali lenye kutaka ku-reveal utambulisho, wengine wanaweza kuanzia hapo kuunga nukta hivyo sikuona ni busara.

Amani mlamu!
 
Ni sawa kwa vile kaamua kukujibu, ni kwa ujasiri wake na amesema anajiamini. Ila mi niliona ni swali lenye kutaka ku-reveal utambulisho, wengine wanaweza kuanzia hapo kuunga nukta hivyo sikuona ni busara.

Amani mlamu!
Nlimuuliza swali ambalo linampa tahadhali sana, kwa nia njema sana maana jina na avatar ni sawa JF na Twitter!
 
Nitakuwa wa mwisho kuamini eti Membe ametoka CCM aje amsindikize Lissu. Kama mnataka Mgombea mmoja basi lazima awe Membe bila hivyo ninachokiona mda si mrefu ACT na CDM wanaanza kuparuana!
 
Mawazo yako yanaanza na kuenguliwa, halafu unaita wengine wavivu wa kufikiri

Kama.una adui mkubwa nafsini kwako, ni kuona kila.fikra zako ziko deep kuliko za wengine
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kuna logic! Kama wana nia ya kuungana, ni matter ya mmoja kujitoa mwishoni if all two will be certified! , this also can work effectively!
Nikuulize, hivi Britanicca wa Twitter ndio wwe?
Labda asirudishe fomu mmojawapo lakini ukisharudisha fomu ndio imetoka hiyo kujitoa hakutakbuliwi na NEC .Watakuweka mgombea . Mengine ujijua mwenyewe

Na huo Ni mtegi mfano mumekubaliana kisirisiri kuwa wewe chukua fomu ila usirudishe NEC akaamua kurudisha utamfanya Nini? Huna Cha kumfanya
Utabaki unalialia kichinichini tu biashara imetoka na yeye mgombea

Don't trust secret arrangements!!!!
 
Huenda uko sahihi, je ikitokea wote wameidhinishwa na Nec kugombea Urais je mtahamia kwa nani? na kwanini?

Hapo sasa kila mtu atashinda mechi zake.
 

Mkuu uchaguzi wa October ni baina ya Magufuli na vyama vya upinzani. Magufuli kama Magufuli hajawahi kushinda bila mizengwe. Tazama hata mwenendo wa uchaguzi huu, ni dhahiri kanuni zake ni kwa ajili ya kukidhi utashi binafsi wa Magufuli. Hivyo mizengwe ya kiwango cha juu ni lazima. Ndio maana msimamo wetu wa kudai tume huru, uko palepale.
 
Britanicca wewe si ulisema uliacha siasa.

Kumbe ilikuwa kukata tamaa tu kutokana na utendaji mbovu wa ngosha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…