Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Wanawake wawili, wafanyabiashara ndogondogo maarufu kama Wamachinga wakazi wa Wilaya ya Makete, mkoani Njombe wanaofanya shughuli zao ujasiriamali mjini Makambako wamezua taharuki mjini Njombe baada ya kuganda ghafla barabarani wakishindwa kusema chochote na kutembea kwa zaidi ya saa moja huku sababu ikitajwa kuwa imetokana na imani za kishirikina.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo katika eneo la mtaa wa posta Jengo la TRA zamani ambapo amebainisha kuwa akina mama hao ni wakazi wa kijiji cha Lupila wilaya ya Makete lakini wanafanya kazi mjini Makambako.
Kamanda Issa amebainisha kuwa mara baada ya kupata taarifa waliweza kufika na kuwachukua ili kuwafikisha kituo cha polisi lakini mmoja kati yao alitamka neno moja tu YESU na kurudi katika hali ile ile ambapo iliwalazimu kuwapeleka hospitali ambapo madaktari walibainisha kuwa watu hao hawana tatizo lolote la kiafya.
Baadhi ya Mashuhuda wa mkasa huo wamesema waliona wanawake hao wakipita na viatu lakini baada umbali mfupi wakasimama ghafla huku wakishindwa kuongea wala kusogea na pale ambapo watu walijaribu kuwatikisa walikuwa wakilia huku wakitamka maneno Moto Moto!