KERO Wanaoendesha pikipiki zenye milio ya juu usiku wa manane maeneo ya Ilala Boma hadi Buguruni ni kero, wachukuliwe hatua

KERO Wanaoendesha pikipiki zenye milio ya juu usiku wa manane maeneo ya Ilala Boma hadi Buguruni ni kero, wachukuliwe hatua

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
276
Reaction score
473
Ni muda sasa wakazi wengi wa maeneo Ilala ikiwemo boma, Amana, Bungoni, Sharifu Shamba, Malapa na Buguruni Rozana tunateseka na kero ya wanaoendesha pikipiki zenye milio ya juu wakati wa usiku tukiwa tumelala.

Kero hii inatokea kuanzia majira ya saa sita usiku hadi kwenye saa nane wakati mwingine mpaka saa tisa , ambapo baadhi Watu jamii ya wahindi ambao wengi wao wanaishi Mjini Posta na Kariakoo ikifika majira hayo, wanasogea pale China Plaza karibia na Karume wanaanza michezo yao ya kukimbiza pikipiki ambazo ni maarufu kwa kuinuka juu na kutoa milio mithiri ya mabomu yanayolipuka.

Nilipofuatilia kujua kwanini wamekuwa wakipendelea njia hiyo, nikabaini ni kwa sababu barabara hiyo haina bampsi, hasa kuanzia eneo la China Plaza kuelekea Buguruni, jambo ambalo ni rafiki kwao kufanya michezo yao.

Hali hiyo imekuwa ikituondolea utulivu wa kupunzika wakati wa usiku kutokana na kila baada ya muda milio milio, hata watoto wetu wadogo hawapati fursa ya kulala usingizi vyema inavyotakiwa.

Lakini kibaya zaidi miongoni mwa maeneo ambayo nadhani nayo yanaathiriwa na milio hiyo ni Hospitali ya Amana, milio ya aina hiyo kwa mgonjwa ambaye anahitaji mazingira ya utulivu hawezi kuupata kwa hali hiyo.

Tunajiuliza mamlaka ziko wapi jamani, kushindwa kuiona kero hiyo na kuchukua hatua, basi kama hawajagundua tunaomba malalamiko yetu yawafikie na mchukue hatua kutuondolea kero hiyo inayotulaza macho.

images - 2024-08-02T100541.561.jpeg
 
Naunga mkono hoja, hata wale wa mchana bodaboda wana vidubwasha vyao vinatowa mlio kama wa bunduki nao washungulikiwe, honi kama za heav duty truck wakati ni bodaboda pia washughurikiwe.
 
Back
Top Bottom