Wanaofanya sherehe za madarasa mapya wakati wapo kwenye msiba wa kufelisha nawashangaa

Wanaofanya sherehe za madarasa mapya wakati wapo kwenye msiba wa kufelisha nawashangaa

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2016
Posts
2,668
Reaction score
3,751
Miaka ya hivi karibuni viongozi wa umma wameingiwa na tabia ya kusifu na kushangilia hovyo.

Kupitia mitandao ya kijamii tunashuhudia wakurugenzi na wakuu wa wilaya wakijisifia ujenzi wa madarasa kana kwamba nikitu ambacho hakikua kinawezekana.

Hao hao viongozi wameandamwa na msiba wa shule za umma kufelisha ikilinganishwa na zile za binafsi.
Kupitia mitandao ya kijamii sijaona hata mkurugenzi mmoja au mkuu wa wilaya aliyegusia huu msiba mzito wa watoto kupata zero.

Viongozi badilikeni acheni tabia ya kusifiasifia mambo ya kawaida hata pale ambapo mtu anatimiza wajibu wake. Ujenzi wa madarasa nijukumu la serikali. Kwanini mnasifu kupita kiasi kana kwamba mmeoewa msaada kutoka jamii nyingine?

Nimeshangaa sana kuona eti mkurugenzi anaingia darasani na kuanza kusema mama Samia Suluhu hoyeeeee wanafunzi wanaitikia......hii ilikua mkoani kagera nadhani. Hili limekaa kisiasa zaidi kuliko kitaaluma.

Watanzania tubadilike. Tuache ushabiki wenye lengo la kuneemesha na kupalilia zaidi teuzi hata pale pasipo stahili.
Viongozi sasa baada ya kujenga madarasa mjipange watoto wapate elimu bora na zero zipungue kwa kiasi kikubwa kama sio kuisha.

Hebu jutieni hizo sifuri ambazo hata nyie mnao mchango hata kwa asilimia ndogo
Msijitoe ufahamu kufanya sherehe ya madarasa wakati manao msiba wa kufelisha. Badilikeni
 
Mh mama Samia suluhu Hassan oyeeeeeeeeeeee .......
 
Wakiwa mezani wanakula Hawataki kusikia hizi habari
 
IMG_20211219_101743_1.jpg

Kama hili unaachaje kufanya sherehe
 
Back
Top Bottom