KERO Wanaofanya usafi barabara za Dar hawaondoi uchafu bali wanauhamisha

KERO Wanaofanya usafi barabara za Dar hawaondoi uchafu bali wanauhamisha

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Hili sijui ni la Waziri wa Afya ama mazingira ama wote wawili?

Kuna uchafuzi mkubwa sana kwenye barabara za Dar es Salaam pamoja na mifereji na mitaro yake unaofanywa na makampuni yaliyopewa kandarasi za kusafisha barabara za jiji mitaro na mifereji yake na wahusika wala hawagutuki ama kuchukua hatua.

Je hii inatokana na kupeana kandarasi kwa kujuana ama kwa rushwa? Wafanyakazi wa makampuni husika wanapofagia michanga barabarani hukuisanya na kuihamishia kwenye hifadhi na kingo za barabara ambazo nyingine zina bustani nzuri za maua.

Wafanyakazi wa makampuni husika wanaposafisha mitaro na mifereji pembezoni mwa barabara lile tope hurundikwa pembezoni, kingoni na kwenye hifadhi za barabara mifereji na mitaro
Matokeo yake ni nini?

Ni kuharibu mandhari nzuri za hifadhi za barabara zenye bustani nzuri kuchafua na kuharibu kingo za barabara
Kuchafua na kuharibu mitaro na mifereji iliyojengwa kwa gharama kubwa. Kutengeneza vilima vya uchafu kwenye hifadhi za barabara, mifereji na mitaro.

Soma Pia: Kariakoo kuna chemba zinatema maji machafu na kuhatarisha afya za Watu, Viongozi wapo kimya

Kusababisha baadhi ya mitaro na mifereji kufurika ama kuziba wakati wa mvuta kutokana na uchafu mwingi uliowekwa pembezoni kurudi kwenye mtaro ama mfereji, Kusababisha magonjwa ya milipuko hasa nyakati za mvua.

Wakandarasi wanaopewa hizi tenda wanalipwa pesa za, Kufagia, Kusafisha, Kukusanya na kwenda kutupa taka ama uchafu kwenye maeneo rasmi yaliyotengwa kwa shughuli hizo. Kinachoshangaza ni kwamba huo mtiririko wa hizo Kazi haifanyiki kwa usahihi na kwa ukamilifu pengine kutokana na uzembe, uvivu, kutojali, kutofuatiliwa
Ukosefu/uhaba/uhafifu/uchache wa vitendea Kazi na wafanyakazi mahiri wenye ujuzi

Mamlaka husika zipo zinaona, wahusika wapo, wakaguzi wapo lakini hakuna uwajibikaji hata kidogo na kila mwisho wa tenda mtu hupewa hati safi, kulipwa na kupewa tena tenda nyingine mpya! Hii kero iwafikie washika dau Wote. Wizara ya afya, Wizara ya mazingira (kama ipo), Mamlaka ya jiji, Serikali za mitaa Wakandarasi wa usafi, Wananchi katika ujumla wao!

Nawakilisha!
 
Tenda zote hizo za Halmashauri na Majiji zinafanywa na viongozi wanaotoka kwenye Baraza la Madiwani. Ni mirija ya watu hiyo. Kikubwa warekebishe hayo mapungufu ila hizo tenda hata NEST hazitangazwi
 
Tenda zote hizo za Halmashauri na Majiji zinafanywa na viongozi wanaotoka kwenye Baraza la Madiwani. Ni mirija ya watu hiyo. Kikubwa warekebishe hayo mapungufu ila hizo tenda hata NEST hazitangazwi
Wakitanguliza masilahi ya taifa mbele itawezekana kabisa .. Kinyume cha hapo huo uozo hautakaa uishe
Wao wanatanguliza maslahi yao mbele na wafanyakazi wao kwenye hizo kandarasi wanafanya hivyohivyo
Gari ya taka inatakiwa kukusanya taka zinazofagiliwa na kupeleka dampo mara 5 kwa wiki, boss anakata siku mbili wakati kwenye tenda kalipwa siku 5
Msimamizi wa site anakata siku moja
Dereva naye anachakachua mafuta ... Matokeo yake ni uchafu kurundikwa bila kupelekwa maeneo husika
 
Nimependa sana, inasikitisha.
Kama kuna wenzangu na mimi, ambao ulifika jijini ukawa wa traffic jam na wa Mama wanafagia unajikuta unawaangalia wao na fagio lao
👇🏽👇🏽👇🏽
Kliki Thanks
 
Jambo la msingi sana umeliona. Pia hizo kazi au vibarua walitakiwa wapate wanachuo au wanafunzi wawe wanalipwa kwa kufanya usafi ili wapate pesa za kujikimu pia kujifunza umuhimu wa usafi wa mazingira viende sambamba na kupewa vitendea kazi bora kama mabuti, gloves, miwani, kofia ngumu, mask n.k na muda wa usafi ufanyike mida ya usiku au alfajiri wakati pilika pilika na mishemishe hazijawa nyingi.
 
Back
Top Bottom