Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Bandiko hili ni angalizo nililitoa kitambo, kuwa wanaohamia CCM wasibezwe!. Makamanda waliokuwa Chadema na kuhamia CCM sasa ndio wanakwenda kuwa mwiba kwa upinzani
P
Mabibi na mabwana, heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Wahenga walisema staajabu ya Mussa lakini siyo ya Firauni.

Je, huyu si ndiye aliyemtuhumu jiwe kununua wabunge?

View attachment 1575679
Ama kweli staajabu ya Mussa!
Endelea kustaajabu, kwa taarifa tuu na kukusaidia, Joshua Nasari, amejitambua na kuchukua hatua kwa kujiunga na the best party in Tanzania!.
P
 
Pascal Mayalla kweli waliona mbali? Wasibezwe? You are very myopic. Ndiyo maana tunasema political science is not pure science as it involves human variable which is unpredictable
 
Hii kitu bado kinaendelea akili kwa pascal au umebadilisha mawazo ??
Mpaka tuna kila sababu zikuwadharua watu walioamia CCM, hakuna faida yeyote ile waliyopata zaida ya hasara.
Tukianza na wabunge wote walioama, kila mtu anajua wajumbe waliwafanya nini na hata hao ambao walifanikiwa kupita kwa kubebebwa na JPM bado hali zao siyo za kujivunia kama wanauhakika wakushinda kula kwenye uchaguzi huu.
Kwa mtazamo wangu naona chadema imekuwa na nguvu zaidi, na CCM imefanya funzo kubwa sana kwa vijana wenye tamaa na uchu wa madaraka, matumaini yangu uchaguzi zijazo viongozi wateule hawatakuwa teyari kuunga juhudi tena.

pascal upo kimya sana kwenye uchaguzi huu, au ndio umeamua kukata mkia wako ili kusubiri nafasi za vitu maalum kama mzee akishinda? Mzee hatashida kaka, wewe endelea kuwa huru na bora ujipendekeze kwa chadema sasa kwani wanao uhakika wa kuchukua dola hapa 28 OCTOBER.
 
Kwa sababu tarehe 28 October, Watanzania tunakwenda kufanya uamuzi, sasa muda huu kabla ya uchaguzi, najifanyia tathmini nilisema nini kuhusu uchaguzi huu, na baada ya matokeo, nitarejea na kupima kilichotokea na nilichokiona kabla.
Natoa wito kwa Watanzania wenzangu, tujitokeze kwa vingi kupiga kura na kuchagua chama, viongozi tunaowataka ambao watatuletea maendeleo ya kweli. Kwa wanaotaka maendeleo ya kweli, watachagua chama na maendeleo ya kweli, lakini kwa wanaotaka porojo tuu, rukhsa kuchagua porojo ni haki yako ya kidemokrasia kuchagua chama chochote, kiongozi yoyote.
Paskali.
 
hopeless kabisa
 
Mkuu Mr.mzumbe , haya bana na tusubiri matokeo
P
 
Sina uhakika wangapi humu walisoma hoja za bandiko hili na kuzielewa!. Kwa wale wanaoshangaa matokeo ya uchaguzi huu, wajikumbushe hoja hizi.
P
 
Sina uhakika wangapi humu walisima hoja za bandiko hili na kuzielewa!. Kwa wale wanaoshangaa matokeo ya uchaguzi huu, wajikumbushe hoja hizi.
P
Hili ni la wazi lakini uwezo wa Magufuli kuipeleka Tanzania level za China ni wa kutilia shaka. Yuko busy kujenga misingi ya kulinda siasa za CCM na si kujenga mifumo ya kazi ambayo China imewapaisha. Uzalishaji mdogo na uchumi mdogo utaturudisha kuhitaji mbadala unless mrithi wake aboreshe hiyo sehemu.


Kwa sababu hii pia siasa za upinzani za matembezi na kutegemea msaada nje zitajifia. Na wale wapinzani maarufu wa tangu 1995 hii ni mara ya mwisho kwao kimantiki.
Endapo kutaibuka sura mpya za wahanga wa mfumo huu, nazungumzia kizazi ambacho wana miaka 25-35 kwa sasa zinaweza kubadilisha trend za 2025.
Pamoja na kushindwa upinzani bado wana karibu nusu ya kura halisia.

Pamoja na hayo, sisi bado tunategemea upepo wa dunia na Afrika. Ikiendelea huko kwingine hali basi fikra zake zitadumu.

Pia endapo akiweza kuweka mifumo ya kazi ambayo itatuhakikishia fursa za maisha bila kujihusisha na siasa basi atakuwa amefanikisha ndoto yake ya kuelekea China.
 
Sina uhakika wangapi humu walisima hoja za bandiko hili na kuzielewa!. Kwa wale wanaoshangaa matokeo ya uchaguzi huu, wajikumbushe hoja hizi.
P
Nimekusoma mkuu..kwa hiyo tutegemee maendeleo ya kiwango cha juu sio? Kuna haja hata ya kufuatilia bunge lijalo? Kama ndivyo tutakua tunafuatilia nini?
 
Pia endapo akiweza kuweka mifumo ya kazi ambayo itatuhakikishia fursa za maisha bila kujihusisha na siasa basi atakuwa amefanikisha ndoto yake ya kuelekea China.
Mkuu double R , kwanza asante kwa objectivity yako, hili la kujenga mifumo, systems, naungana na wewe asilimia 100% kwa 100%. Mimi pia niliwahi kulizungumzia hapa,
P
 
Mkuu Kituko , hapa ni katika kukumbushana tuu, hoja hii niliirudia hapa
Naamini umeona kilichotokea!.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…