Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?

Naendelea tuu kusisitiza, hawa watu wanaohamia CCM, wasibezwe!, wanaona mbali!.
P.

Shukrani Pascal kwa utabiri makini kwani ni kweli wote wameona mbali na hawakuishia hapo tu bali pia wamesikia na kunusa kuwa 2020 hakutakuwa na mgombea wa CDM wala ACT hivyo kwanini wasianze kuchanga karata zao sasa hivi? amini usiamini zoezi linaendelea lakini pia baadhi yao wataambulia "karamu ya fisi"
 
Haya endelea kutafuta kiki, matokeo ya serikali za mitaa yatakufungua macho, mwaka 2020 ni funga kazi.
Ni ukweli ulio dhahiri kuwa vyama vya upinzani havikujiandaa kufanya siasa katika mazingira kama ya sasa ambapo chama kilicho madarakani pamoja na mapungufu yake lakini kinatekeleza kwa asilimia kubwa yale ambayo wao walikuwa wanayapigia makelele.

Ni lazima sasa watafute strategy la sivyo baada ya october 2020 litakalotokea litakuwa historia nyingine kubwa.
 
Strategy mpya dhidi ya mtu anayewatuma watendaji kuharibu form za wagombea wa upinzani ni strategy inayosimamia madai ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
 
"hongera kubwa zaidi ambayo ni hongera in advance ni ya uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 ambapo CCM itakomba kila kijiji na kila mtaa".......


nimenukuu sehemu ya sentensi kwenye aya yako ya mwisho ya bandiko hili la Nov 2017 exactly 2yrs ago!..... bravo paskali,bravo!


but one thing is for certain "we are doomed"....... but i can bet wabunge wakatoliki waliopo upinzani 2020 wanaweza kurudi bungeni kama wakigombea kupitia upinzani ila hawa wa matengenezo sijui protestant wasahau!
 
Mkuu umenena vizuri. Anacho maanisha Pascal ni kuwa ccm itashinda kwa njia ovu kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa marudio. Jambo asilolijua ni kuwa siasa hazitabiriki na mwaka ujao utakuwa mwaka wa maajabu sana. Ukweli ni kuwa JPM hakubaliki kabisa ndiyo maana wakaanda mbinu chafu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa
 
Kwa maoni yangu mimi kama lengo la Taifa letu ni kujenga Taifa lenye mfumo wa chama kimoja kinachofanyika sasa hivi ni sawa kama lengo ni lile liloandikwa kwenye katiba kwamba Tanzania ni nchi yenye mfumo wa vyama vingi na kwamba lengo la Taifa ni kuiimalisha mfumo huu kinachofanyika si sawa kwa sababu ni tofauti na malengo yetu tuliyo ya documents kwenye katiba na sheria nyingine za nchi labda njia bora ni kubadilisha malengo ya kitaifa
 


Kuna matatizo mawili yatatokea
1. Kwasababu upinzania utashidwa kwa kusisia na sio kwenye mioyo ya watu imebadilika upinzania utaendelea. Kuna tofauti kubwa kati ya upinzani na vyama vya siasa.
2. Watu wengi wameenda kimaslahi na si kweli kwasababu ya kuunga mkono maana kuna Watanzania wengi kama sisi hatuna vyama. Hivyo kuna hatari upinzani kutawaliwa na matajiri kuloko ilivyo sasa
3. Upinzania utabadilika miaka ijayo na utakuwa upinzania wa kupigania uhuru kama ulivyo huko Sudani na sio upinzania wa kupigania maendeleo. Kuna tofauti. Hii itakuwa ngumu kwa CCM maana maendeleo yatazoeleka lakini watu watahitaji uhuru mfano Bolivia president aliingia hivi hivi baada ya watu kuzoea maendeleo wameandamana na kumtoa kakimbilia Mexico ingawa ndiye kaleta maendeleo

 
Can't shy away from tribalism Pasco ! Ndio maana Nyerere hakuwapa vyeo! Nakumbuka Ilboru ulivyokuwa. You are what you have always been
 
Can't shy away from tribalism Pasco ! Ndio maana Nyerere hakuwapa vyeo! Nakumbuka Ilboru ulivyokuwa. You are what you have always been
Mkuu Nyani Mzee, kumbe ulisoma Ilboru?. Hongera, maana kusoma Ilboru sio mchezo, ila kuniita mimi ni mkabila tangu Ilboru, ni uthibitisho kuwa wewe ulihadithiwa tuu kuwa Pasco Mayalla alisoma Ilboru, ila utakuwa hunijui kabisa!.
P
 
Paskali huwa unaona mbali sana!!
 
Ni watu waliojaa mavi tu akili zao ndio wanaona hivyo
Dah...kwa akili ndogo tu...isiyohitaji hata digrii... Kazi ya siasa ndiyo inawafanya wajaze matumbo yao...Ni Kama banker anayeona benki yake inaenda kufilisika [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…