Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Tokea kujiudhuru kwa aliyekua mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji mambo ndani ya klabu hiyo yameendelea kuwa ovyo baada ya kundi la wajanja wachache kutumia nafasi hiyo kupiga hela nje nje.
Jezi mpya za Yanga zinazotengenezwa na mshonaji nguo Speshoz kupitia jina la Bongoz zinauzwa kama njugu kwa wanachama wasiojua kuwa klabu yao haipati chochote.
Jezi hizo ni mpango wa mjumbe wa kamati ya utendaji, Salum Mkemi ambaye awali Manji alimsimamisha uanachama wake kabla ya kurejeshwa na Katibu Mkuu Mkwasa, anauza jezi hizo kama njugu kwa bei ya elfu 35 kwa pea moja, na mauzo ya jezi hizo anajua yeye mwenyewe Mkemi anakopeleka.
Biashara hiyo inafanyika hadharani, viongozi wa Yanga wanatazama kiongozi mwingine akijipatia fedha ambazao kama zingeingia kwenye mfuko wa klabu basi zingeweza kusaidia matatizo madogo madogo ya kiutawala.
Duniani biashara ya jezi ndo huviingizia mapato makuba vilabu, lakini kwa Tanzania ni tofauti wanaofaidika ni wengine kupitia majina ya taasisi hizo, kidogo Simba na Azam wamepiga hatua kwa kufungua maduka yanayouza vifaa vyao.
Wakati hilo la jezi likiwa na takribani miezi mitatau sasa tangu kuanza kuuzwa, watendaji wengine wameendelea kudaia percent kwenye usajili wa wachezaji.
Salim Hoza aliyetua Azam alikubaliana na uongozi wa Yanga kusaini kandarasi ya kuitumikia kwa makubaliano ya kutanguliziwa mil 5 kisha kumaliziwa baadae pesa yake nyingine ya usajilli, ajabu mtu anaefahamika kama Godlisten Chacharito alipewa jukumu hilo na kumpa Hoza mil 4.5, akizuia laki 5, hali iliyomfanya mchezaji huyo kuamua kutimikia Azam kimya kimya.
Mwaka jana Yanga ilipigwa faini kwa kuchelewa kukamilisha usajili na TFF baada ya kumalizika siku 68 za usajili ilijikuta haijafanya usajili kwenye mtandao na kama si huruma ya TFF basi timu hiyo ilipaswa kushushwa daraja na si kutozwa fainai.
Aliyekua Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Desdeudit alishidwa kufanya usajili wa Hassan Kessy pia ukiwa na pingamizi liliopelekea mchezaji huyo kuchelewa kuitumikia Yanga mpaka kesi yake ilipotolewa uamuzi na kamati husika, kwa kupigia faini Yanga kwa kumsainisha mchezaji mkataba ili hali mkataba wake ukiwa haujamalizika.
Baada ya Niyonzima kushindwana na uongozi wa Yanga jumatatu usiku, uongozi ulipanga kutoka taarifa kwa umma mapema juu ya suala hilo, lakini kabla hilo halijafanyika Baraka Desdeudit alimpigia simu Niyozima na kumuambia asajili Simba haraka, kwani kuna mpango wa kukutangaza kuwa tumekuacha.
Kwa maana hiyo Niyonzima alisaini haraka Simba kuogopa kutangazwa katemwa, sababu kungemshushia hadhi yake, ila aliyetoa siri hii kwa mchezaji huyo ni Baraka Desdeudit ambaye hata mie kwa sasa sielewi cheo chake ndani ya Yanga ni nani, maana alikua akikaimu Ukatibu, kabla ya Mkwasa kuajiriwa.
Wana Yanga naomba tujulishwe nafasi ya Chacharito na Baraka Desdeudit ndani ya klabu, maana vyeo vyao havijulikani na inasadikika ni mamluki wanaotumika kuidhofisha Yanga.
Ni ukweli usiofichika, mpaka sasa Yanga haijafanya usajili wa maana, Niyonzima kaondoka, Kamusoko, Bossou, Ngoma, Oscar, Barthez mikataba yao imemalizika, wakati viongozi wengine wakihangaika kwa chochote walicho nacho kuweza kuwapata wachezaji hao, wanapopewa jukumu hilo wanageuka madalali.
Kutoka kwenye ushangiliaji mpaka kupewa majukumu makubwa ya usajili ndani ya Yanga hiki ni kituko kingine, anapata wapi staha kama alikua mshabiki muongea ovyo? Yanga haina siri tena kutokana na kila aliyepo kutaka kuonekana anajuana sana na wachezaji, viongozi wakati uhalisia ufanisi wa kazi hakuna,
Taarifa za klabu ya Yanga sasa zinapatikana kwenye mitandao yao (blogs) na akaunti zao binafsi Instagram, twitter na facebook, whatsapp wana Yanga wangapi wanaweza kupata taarifa hizo kwa kusoma kwenye akaunti zao?
Aah ngoja niishie apa kwa leo, kwa aina hii ya viongozi hao waliopo klabu ya Yanga kwa sasa sioni maendeleo yoyote, kama maendeleo ni Ubingwa wa Ligi Kuu si sawa, sababu ubingwa huo ulishachukuliwa zaidi ya mara 27.