Wanaoihujumu Yanga ni Bwana Chacharito, Baraka Desdeudit na Salum Mkemi

Wanaoihujumu Yanga ni Bwana Chacharito, Baraka Desdeudit na Salum Mkemi

Punguzeni majungu,Niyonzima ameondoka sababu Simba wamempa dau kubwa kuliko Yanga.Dr Tiboroha aligombana na Niyonzima na ndio alitaka kumuondoa Niyonzima Yanga Manji akaingilia kati na kumfukuza,leo mnaleta story Dr Tiboroha ndio ammempeleka Niyonzima Simba

Naamini tunapita katika wakati mgumu ila mambo yatatulia
 
Punguzeni majungu,Niyonzima ameondoka sababu Simba wamempa dau kubwa kuliko Yanga.Dr Tiboroha aligombana na Niyonzima na ndio alitaka kumuondoa Niyonzima Yanga Manji akaingilia kati na kumfukuza,leo mnaleta story Dr Tiboroha ndio ammempeleka Niyonzima Simba
Usiwe na haraka, utapata jibu si muda mrefu
 
Huyu kenge si alijifanya kumtimua Niyonzima kipindi flani leo kageuka malaika kwa Niyonzima dah
Huyo ni mpiga dili kama wengine tu. Hivi sasa yupo beneti na Kaburu kuiumiza Yanga
 
Ya kazi gani unafikiri yale mambo ya kukabidhiana hela kama zawadi yapo yanga sasa hivi? Huyo niyonzima mwenyewe kaondoka yanga sbb ya madalali hao mikia wenyewe wanajuta saaa hivi jinsi walivyopigwa baada ya yanga kumpa makavu
Yule hoza alipewa ml 5 hata kaka yake amethibitisha lkn tamaa ya familia ndio iliyoharibu baada ya azam kwenda na dau kubwa zaidi halafu cash sio nusu kama yanga mengine majungu tu na umbea.
Tiboroha ndio kidudu mtu na mnafiki kaka wewe hata msuva alitaka kumpeleka mikia kwa kisingizio anakwenda nje alifikia mpaka kwenda kuvunja mkataba kwa kisingizio cha kutolipwa miezi mitatu akagongwa mwamba baada ya kukuta hakuna madai ya mshahara
Mkuu kumbuka wachezaji hawachezi mpira maisha yao yote na kumbuka kule sio kama ajira zingine kwamba utalipwa mafao ya uzeeni,
Waachane vijana wapige pesa wakati ni wao na wakati ni huu na hao Mikia waache wapigwe ili mradi wenyewe wameridhia.
Haya mambo ya kusema nachezea damu siku hizi hamna hata huyo Msuva amevumilia sana miezi mitatu hajalipwa..?
Ni wachezaji hawa hawa ambao wengi wao tunawaona wakiishi maisha ya dhiki na tabu siku za mbele na kuomba wachangiwe hivyo waachane wapige pesa na ni sisi sisi mashabiki baadae tunaongea pembeni fulani si alikuwa maarufu yule enzi anacheza mpira wakati alikuwa hapati pesa.
All in all wakati una mwisho na hawana mafao hao.
 
Huyo ni mpiga dili kama wengine tu. Hivi sasa yupo beneti na Kaburu kuiumiza Yanga
Niyonzima kaondoka Yanga sababu Simba wamempa signing fee $70,000 kwa mkupuo while Yanga walitaka kumpa $60,000 kwa awamu mbili.Mshahara wa Yanga/Simba wote ulikuwa sawa $3,000
 
Mkuu kumbuka wachezaji hawachezi mpira maisha yao yote na kumbuka kule sio kama ajira zingine kwamba utalipwa mafao ya uzeeni,
Waachane vijana wapige pesa wakati ni wao na wakati ni huu na hao Mikia waache wapigwe ili mradi wenyewe wameridhia.
Haya mambo ya kusema nachezea damu siku hizi hamna hata huyo Msuva amevumilia sana miezi mitatu hajalipwa..?
Ni wachezaji hawa hawa ambao wengi wao tunawaona wakiishi maisha ya dhiki na tabu siku za mbele na kuomba wachangiwe hivyo waachane wapige pesa na ni sisi sisi mashabiki baadae tunaongea pembeni fulani si alikuwa maarufu yule enzi anacheza mpira wakati alikuwa hapati pesa.
All in all wakati una mwisho na hawana mafao hao.
Unajuma maana ya kupigwa? Unafikiri hizo dola elfu 70 ndio dau lake kwa taarifa yako tu madalali wanakula karibu nusu ya hela na ndio kilichofanya yanga waachane nae sbb walitaka kumpa dola 60 elfu lkn 40 cash na 20 kabla ya ligi kuanza lkn kwa sbb madalali wanataka hela wakamshawishi akatae manake lengo lao lisingetimia na kumpanga akachukue za simba ba kule nako walijua atachukua kiasi lkn wakagoma matokeo yake wanakimbizana kukamilisha hela zote na kwa kuingilia bajeti nyingine mpira maisha lkn madau wanayotanga kupewa hawapewi zote
 
Niyonzima kaondoka Yanga sababu Simba wamempa signing fee $70,000 kwa mkupuo while Yanga walitaka kumpa $60,000 kwa awamu mbili.Mshahara wa Yanga/Simba wote ulikuwa sawa $3,000
Mkuu lazima kuna zaidi ya hapo. Haiwezi kuwa issue ya US $ 10,000 tu na malipo ya installments. Miaka yote Yanga wamemlipa kwa hizo installments bila kukosa.
 
Wana yanga tukubali kuwa mambo hayaendi sawa klabun na hasa kipindi hiki cha usajili
 
NAOMBA KINUKE HADI MWISHO WA LIGI IJAYO tuwape 8
 
Wana yanga tukubali kuwa mambo hayaendi sawa klabun na hasa kipindi hiki cha usajili
Tunatakiwa tuwe watulivu sio kushikana uchawi coz ishaeleweka pesa Hakuna, muhimu ni kujiandaa kisaikolojia tu kipindi hiki kigumu
 
Unajuma maana ya kupigwa? Unafikiri hizo dola elfu 70 ndio dau lake kwa taarifa yako tu madalali wanakula karibu nusu ya hela na ndio kilichofanya yanga waachane nae sbb walitaka kumpa dola 60 elfu lkn 40 cash na 20 kabla ya ligi kuanza lkn kwa sbb madalali wanataka hela wakamshawishi akatae manake lengo lao lisingetimia na kumpanga akachukue za simba ba kule nako walijua atachukua kiasi lkn wakagoma matokeo yake wanakimbizana kukamilisha hela zote na kwa kuingilia bajeti nyingine mpira maisha lkn madau wanayotanga kupewa hawapewi zote
Ni nani anapokea pesa za Niyonzima..?
Humu kuna watu wengi wanajifanya wapo karibu na Simba au Yanga na maelezo ya leo yanakuwga tofauti na waliyoyatoa jana au ambayo watatoa kesho
 
Ny
Tokea kujiudhuru kwa aliyekua mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji mambo ndani ya klabu hiyo yameendelea kuwa ovyo baada ya kundi la wajanja wachache kutumia nafasi hiyo kupiga hela nje nje.

Jezi mpya za Yanga zinazotengenezwa na mshonaji nguo Speshoz kupitia jina la Bongoz zinauzwa kama njugu kwa wanachama wasiojua kuwa klabu yao haipati chochote.

Jezi hizo ni mpango wa mjumbe wa kamati ya utendaji, Salum Mkemi ambaye awali Manji alimsimamisha uanachama wake kabla ya kurejeshwa na Katibu Mkuu Mkwasa, anauza jezi hizo kama njugu kwa bei ya elfu 35 kwa pea moja, na mauzo ya jezi hizo anajua yeye mwenyewe Mkemi anakopeleka.

Biashara hiyo inafanyika hadharani, viongozi wa Yanga wanatazama kiongozi mwingine akijipatia fedha ambazao kama zingeingia kwenye mfuko wa klabu basi zingeweza kusaidia matatizo madogo madogo ya kiutawala.

Duniani biashara ya jezi ndo huviingizia mapato makuba vilabu, lakini kwa Tanzania ni tofauti wanaofaidika ni wengine kupitia majina ya taasisi hizo, kidogo Simba na Azam wamepiga hatua kwa kufungua maduka yanayouza vifaa vyao.

Wakati hilo la jezi likiwa na takribani miezi mitatau sasa tangu kuanza kuuzwa, watendaji wengine wameendelea kudaia percent kwenye usajili wa wachezaji.

Salim Hoza aliyetua Azam alikubaliana na uongozi wa Yanga kusaini kandarasi ya kuitumikia kwa makubaliano ya kutanguliziwa mil 5 kisha kumaliziwa baadae pesa yake nyingine ya usajilli, ajabu mtu anaefahamika kama Godlisten Chacharito alipewa jukumu hilo na kumpa Hoza mil 4.5, akizuia laki 5, hali iliyomfanya mchezaji huyo kuamua kutimikia Azam kimya kimya.

Mwaka jana Yanga ilipigwa faini kwa kuchelewa kukamilisha usajili na TFF baada ya kumalizika siku 68 za usajili ilijikuta haijafanya usajili kwenye mtandao na kama si huruma ya TFF basi timu hiyo ilipaswa kushushwa daraja na si kutozwa fainai.

Aliyekua Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Desdeudit alishidwa kufanya usajili wa Hassan Kessy pia ukiwa na pingamizi liliopelekea mchezaji huyo kuchelewa kuitumikia Yanga mpaka kesi yake ilipotolewa uamuzi na kamati husika, kwa kupigia faini Yanga kwa kumsainisha mchezaji mkataba ili hali mkataba wake ukiwa haujamalizika.

Baada ya Niyonzima kushindwana na uongozi wa Yanga jumatatu usiku, uongozi ulipanga kutoka taarifa kwa umma mapema juu ya suala hilo, lakini kabla hilo halijafanyika Baraka Desdeudit alimpigia simu Niyozima na kumuambia asajili Simba haraka, kwani kuna mpango wa kukutangaza kuwa tumekuacha.

Kwa maana hiyo Niyonzima alisaini haraka Simba kuogopa kutangazwa katemwa, sababu kungemshushia hadhi yake, ila aliyetoa siri hii kwa mchezaji huyo ni Baraka Desdeudit ambaye hata mie kwa sasa sielewi cheo chake ndani ya Yanga ni nani, maana alikua akikaimu Ukatibu, kabla ya Mkwasa kuajiriwa.

Wana Yanga naomba tujulishwe nafasi ya Chacharito na Baraka Desdeudit ndani ya klabu, maana vyeo vyao havijulikani na inasadikika ni mamluki wanaotumika kuidhofisha Yanga.

Ni ukweli usiofichika, mpaka sasa Yanga haijafanya usajili wa maana, Niyonzima kaondoka, Kamusoko, Bossou, Ngoma, Oscar, Barthez mikataba yao imemalizika, wakati viongozi wengine wakihangaika kwa chochote walicho nacho kuweza kuwapata wachezaji hao, wanapopewa jukumu hilo wanageuka madalali.

Kutoka kwenye ushangiliaji mpaka kupewa majukumu makubwa ya usajili ndani ya Yanga hiki ni kituko kingine, anapata wapi staha kama alikua mshabiki muongea ovyo? Yanga haina siri tena kutokana na kila aliyepo kutaka kuonekana anajuana sana na wachezaji, viongozi wakati uhalisia ufanisi wa kazi hakuna,

Taarifa za klabu ya Yanga sasa zinapatikana kwenye mitandao yao (blogs) na akaunti zao binafsi Instagram, twitter na facebook, whatsapp wana Yanga wangapi wanaweza kupata taarifa hizo kwa kusoma kwenye akaunti zao?

Aah ngoja niishie apa kwa leo, kwa aina hii ya viongozi hao waliopo klabu ya Yanga kwa sasa sioni maendeleo yoyote, kama maendeleo ni Ubingwa wa Ligi Kuu si sawa, sababu ubingwa huo ulishachukuliwa zaidi ya mara 27.
Nyie malizaneni tu, sisi TUNAJIPANGA..
 
Mkuu lazima kuna zaidi ya hapo. Haiwezi kuwa issue ya US $ 10,000 tu na malipo ya installments. Miaka yote Yanga wamemlipa kwa hizo installments bila kukosa.
Huko nyuma Simba hawakuwa na ubavu kusajili wachezaji Yanga/Azam sababu hawakuwa wanashiriki michuano ya kimataifa+hawakuwa na fedha while msimu huu imewezekana sababu Simba watacheza michuano ya kimataifa+ wana fedha(MO Dewji +Sport Pesa+Friends of Simba) na Azam/Yanga hakuna fedha , Niyonzima ameshuhudia msimu huu wachezaji walivyopata taabu kulipwa mishahara baada ya Manji kuondoka na kumbuka Niyonzima ameshinda almost kila ubingwa akiwa na Yanga so hakuna motivation ya kuendelea kubaki kama anapata offer nzuri
 
Back
Top Bottom