Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Siku mbili tangu raisi Bashar Al Assad aondolewe madarakani kutokana na upinzani ulioongozwa na wanamgambo wa chamba cha Hizbu Tahrir,dalili zote zinaonesha watu hao wanaoingia madarakani si vibaraka wa Marekani wala wa Israel.
Mataifa hayo mawili inaonekana yalipigwa chenga sana na harakati za wapinzani hao wa Syria ijapokuwa malengo ya harakati hizo hayajawekwa wazi sana.
Ujumbe wa mwanzo alioutoa Abu Muhammad Aljolan ndani ya msikiti wa Ummayad unamuonesha kiongozi huyo si mtu wa visasi na amekusudia kuijenga upya Syria,Wakati huo huo hajatoa dalili yoyote ya kukubaliana na baadhi ya mambo ambayo yanafanywa na nchi za Marekani na Israel ndani ya ardhi ya Syria.
Mwanzoni Israel ilitumai kuondolewa kwa Bashar kutakuwa kumewalemaza Hizbullah na kwamba itakuwa imepata mteremko katika vita vyake na Lebanon,Lakini mbinu iliyotumika Gaza kuundwa umoja wa vyama kupigana na Israel unaweza ukatumika baina ya wapiganaji wa Hizbu Tahri na wenzao kuwaunga mkono Hizbullah kuendeleza vita na Israel.
Hali hiyo ni uchuro kwa Israel na inakera kuisikia lakini ndio itakayoiondolea Israel kuwa kijogoo wa mashariki ya kati.
Mtazamo huo tayari umeishtua Israel ambapo tangu juzi imekuwa ikipiga na kuharibu mali na miundombinu ya kijeshi ya Syria jambo ambalo tangu siku ya mwanzo Aljolani amelikataza na kulilani kufanywa na wapiganaji wake.