Wanaokataa uchawi haupo na bado wanaenda makanisani na misikitini wana dini za utambulisho na kuzugia tu

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Kuna watu ni wabishi sana kwamba haya mambo hayapo lakini utawakuta kanisani ama msikitini wakijinadi wao ni wakristo/waislam. Niseme tu kwamba hapa ni ishara ya moja kwa moja wapo kwenye dini kama kushabikia timu za mpira na wala hawajui elimu ya dini yao.

Mbaya zaidi hawanaga imani, maji yakizidi unga hawa uvumilivu, ndio huwa wakwanza kukimbilia kwa waganga wale matapeli wa kwenye matangazo ya nguzo.

Kwenye Biblia na Quran kote haya mambo yapo. Kwenye Biblia mfano mojawapo, wapo walioweza kuzigeuza fimbo zao ziwe nyoka kichawi zipambane na fimbo ya Musa.

Kwenye Qurani kuna hadithi kwamba Mtume Muhamad alipigwa kipapai ilibaki kuwa jumla jumla lakini alijinasua.
 
Wengine kanisani wanaenda ili kuchangamana na watu mbali mbali hivyo hwafahamu biblia kwa undani
 
Kanakwamba kuna watu ni wabishi sana kwamba haya mambo hayapo lakini utawakuta kanisani ama msikitini ama wakijinadi wao ni wakristo / waislam, Niseme tu kwamba hapa ni ishara ya moja kwa moja wapo kwenye dini kama kushabikia timu za mpira na wala hawajui elimu ya dini yao.

Mbaya zaidi hawanaga imani, maji yakizidi unga hawa uvumilivu, ndio huwa wakwanza kukimbilia kwa waganga wale matapeli wa kwenye matangazo ya nguzo

Kwenye biblia na korani kote haya mambo yapo,

Kwenye biblia mfano mojawapo, wapo walioweza kuzigeuza fumbo zao ziwe nyoka kichawi zipabane na fimbo ya Musa

Kwenye Kurani kuna hadithi kwamba Mtume muhamad alipigwa kipapai ilibaki kuwa jumla jumla lakini alijinasua,
Kama uchawi haupo, haupo tu.

Watu wakienda msikitini na kanisani utakuwa haupo.

Wasipoenda utakuwa haupo.

Kwa hivyo tujadili hoja ya msingi, uchawi upo au haupo?

Uchawi ni nini?

Utajuaje huu ni uchawi na huu si uchawi?

Utajuaje unachofikiri ni uchawi ni uchawi kweli na si kingine usichokijua tu?

Hayo mambo ya msikitini na kanisani hayana maana sana.

Kwa sababu kuna wengine hatuna dini na tunasema habari za kuamini uchawi ni ujinga tu.
 
Kuna movie moja character wa Ice Cube alisema kanisani ndiyo sehemu bora kabisa ya kutafuta totoz!

Kwa hivyo msione watu wanakwenda kanisani mkafikiri wote waumini.

Wengine wanafuata totoz tu.
 
Kama uchawi haupo, haupo tu.

Watu wakienda msikitini na kanisani utakuwa haupo.

Wasipoenda utakuwa haupo.

Kwa hivyo tujadili hoja ya msingi, uchawi upo au haupo?

Uchawi ni nini?

Utajuaje huu ni uchawi na huu si uchawi?

Utajuaje unachofikiri ni uchawi ni uchawi kweli na si kingine usichokijua tu?

Hayo mambo ya msikitini na kanisani hayana maana sana.

Kwa sababu kuna wengine hatuna dini na tunasema habari za kuamini uchawi ni ujinga tu.
Uchawi upo hata ufanyeje labda useme haujawahi kukumbana nao

Narudia kama ni mbongo basi utakuwa sikio la kufa ila uchawi upo na jamii zilishakanywa juu ya mambo ya kichawi

Uchawi na mambo ya kishetani ukisikia freemason ni wachawi ,waganga ,wanaombea wenzao mabaya ,wivu ,chuki vyote ni aina ya uchawi ...

Uchawi ni shirki kumshikirisha Mungu katika mamlaka yake ,uungu wake sifa zake...Sasa hapa Kuna aina nyingi kwa vile huamini Mungu basi tuache .
 
Kanakwamba kuna watu ni wabishi sana kwamba haya mambo hayapo lakini utawakuta kanisani ama msikitini ama wakijinadi wao ni wakristo / waislam, Niseme tu kwamba hapa ni ishara ya moja kwa moja wapo kwenye dini kama kushabikia timu za mpira na wala hawajui elimu ya dini yao.

Mbaya zaidi hawanaga imani, maji yakizidi unga hawa uvumilivu, ndio huwa wakwanza kukimbilia kwa waganga wale matapeli wa kwenye matangazo ya nguzo

Kwenye biblia na korani kote haya mambo yapo,

Kwenye biblia mfano mojawapo, wapo walioweza kuzigeuza fumbo zao ziwe nyoka kichawi zipabane na fimbo ya Musa

Kwenye Kurani kuna hadithi kwamba Mtume muhamad alipigwa kipapai ilibaki kuwa jumla jumla lakini alijinasua,
Uchawi upo hata leo, lakini kuna nguvu kubwa sana ya kuusamaratisha huo uchawi kwa kupitia damu ya Yesu Kristo.
 
Kanisani kuna watu wanaenda ku socialize tu.

Wengine wanakwenda ni kama utamaduni tu wanauenzi. Sababu toka utotoni walikuwa wanaenda na wamezoea kwenda.

Wamekuwa watu wazima na wengine wamepata kazi sehemu nyeti zilizowafanya wajue ukweli kuhusu shetani, Mungu , dini na uchawi. Ukweli wameshaujua ila utamaduni wa kwenda church hawauachi. Ni kama mmasai umzuie kuvaa mashuka akiwa kwao sababu ni tajiri ama msomi.
 
Kama uchawi haupo, haupo tu.

Watu wakienda msikitini na kanisani utakuwa haupo.

Wasipoenda utakuwa haupo.

Kwa hivyo tujadili hoja ya msingi, uchawi upo au haupo?

Uchawi ni nini?

Utajuaje huu ni uchawi na huu si uchawi?

Utajuaje unachofikiri ni uchawi ni uchawi kweli na si kingine usichokijua tu?

Hayo mambo ya msikitini na kanisani hayana maana sana.

Kwa sababu kuna wengine hatuna dini na tunasema habari za kuamini uchawi ni ujinga tu.
Kwani wewe binafsi upo? ( Are you existing or not ?) Maana uwepo wako ni halisi kupitia athari zako ndo tunaamini kuwa upo na unaishi. Athari za uchawi pia ni dhahili mfano mtu kuzaa kobe,kuku,chura.Au mtu kuzikwa na kuonekana baada ya miaka kadhaa akiwa hai. Upepo(Air) hatuuoni wala hatuwezi kuushika lakini athari zake ni dhahili, je tuseme upepo haupo?Ndio maana akitokea mtu anakataa uchawi haupo ni sawa na wewe kukataa kuwa haupo na hauishi.
 
Umeshawahi kushuhudia mtu kazaa kobe au chura?

Mtu aliyezikwa na kuonekana yuko hai miaka kadhaa baadaye jina lake nani? Ulimuona wewe?

Kwani nani kapinga kuwepo kwa upepo?

Upepo unapimwa kwa speed, unapimwa kwa muelekeo, zinachorwa ramani za upepo unavyoelekea, watu wanajua atmospheric pressure inaathiri upepo vipi sehemu gani.

Uchawi unaupima kwa kipimo gani?
 
Back
Top Bottom