SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Katika utafiti mdogo niliofanya hapa Dar es Salaam nimegundua kuwa changamoto za mji huu haziishi na kwa kiasi kikubwa ni zile zile miaka yote kwa kuwa wakaazi wa mjii huu, hasa wale wageni hawataki kubadilika.
Leo nimepita barabara ya Bagamoyo maeneo ya Mbezi, nikaona mdada mmoja anamwaga mihogo mchana kweupe katika njia ya watembea kwa miguu kiasi cha kufunga eneo zima kitendo kitakachowalazimu watembea kwa miguu kuingia barabarani ili kupita eneo lile maana njia ameifunga.
Nikajiuliza, si ni juzi tu kulikuwa na zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wa aina hii? Kuna vituo vya daladala sasa hivi vimegeuzwa ni sehemu za biashara, si machungwa, karanga, matikiti hadi mahindi yanachomwa. Unaweza kuona hali na mbaya kuliko hata kabla zoezi hili lilipofanyika.
Kuna hii dhana ya kuwa tusizibiane riziki. Najua kuna watu watakuja katika uzi huu na mtazamo huo. Lakini kwa mfano nilioutoa wa huyo muuza mihogo, angeweza kabisa kuweka biashara yake upande wa pili bila kubughudhi taratibu na usalama wa wengine, hili ndiyo lilinitatiza. Hawa watu hawaoni tofauti ya shambani na mijini.
Mji huu wa Dar baada ya miaka hii yote, kuna watu wengi sana wamestaarabika na wangependa kuishi katika mazingira ya kistaarabu na yote haya yanawezekana bila kuzuia mtu yoyote kutoka sehemu yoyote kuishi na kufanya biashara zake kwa kufuata taratibu.
Tatizo kubwa ninaloliona ni kuwa wengi wa watu wanaotoka vijijini wanakuja mijini na mitazamo ile ile ya huko walikotoka na wanalazimisha wengine wasalimu amri kwao. Na watu hawa hata wakae Dar miaka 20 hawezi kubadilika maana wakuja wapya wanaendeleza hizi taratibu na hivyo kushinikiza muendelezo wa fikra mbaya.
Nimeleta mada hii huku nikiheshimu harakati za kila mtu za kujitafutia riziki na pia napenda sana mchanganyiko wa mji wa Dar es Salaam ambapo hatuulizani makabila wala tulipotoka ila inahitaji nguvu ya ziada kuleta ustaarabu mjini hapa.
Hawa watu inabidi wakifika Chalinze, washushwe, wakalishwe kama wiki hivi pale wafundishwe taratibu za kuishi mijini zilivyo. Bila kufanya hivyo, huu mji hautabadilika kamwe nawaambia.