Wanaokuja kuishi Dar wapewe semina elekezi

Wanaokuja kuishi Dar wapewe semina elekezi

waondolewe haraka bila kisingizio chochote umasikini isiwe kigezo cha kuvunja sheria na taratibu za nchi
 
Asa izo fedha za tozo ndo zitumike kwenye ushubwadu kama huu usiokua na kichwa wala miguu? Si bora zigharamie madawa uko hospitalini watu wanakufa kwa kukosa dawa.

Halafu unajuaje labda huo unaouona sio ustaarabu kwetu ndo ustaarabu wenyewe huo. Ustaarabu fundisheni watoto zenu uko watakua nao mjini kla mtu yupo na mishe zake za kusaka tonge
Tuishi kama wanyama kisa wewe unasaka tonge? Gharama kubwa zinatumika kujenga miundombinu halafu watu kiholelaholela wanaitumia kwa matumizi ambayo hayajakusudiwa.

Mji ukipangika vizuri wote tutafaidika na tutaishi kwa ustaarabu.
 
Katika utafiti mdogo niliofanya hapa Dar es Salaam nimegundua kuwa changamoto za mji huu haziishi na kwa kiasi kikubwa ni zile zile miaka yote kwa kuwa wakaazi wa mjii huu, hasa wale wageni hawataki kubadilika.

Leo nimepita barabara ya Bagamoyo maeneo ya Mbezi, nikaona mdada mmoja anamwaga mihogo mchana kweupe katika njia ya watembea kwa miguu kiasi cha kufunga eneo zima kitendo kitakachowalazimu watembea kwa miguu kuingia barabarani ili kupita eneo lile maana njia ameifunga. Nikajiuliza, si ni juzi tu kulikuwa na zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wa aina hii? Kuna vituo vya daladala sasa hivi vimegeuzwa ni sehemu za biashara, si machungwa, karanga, matikiti hadi mahindi yanachomwa. Unaweza kuona hali na mbaya kuliko hata kabla zoezi hili lilipofanyika.

Kuna hii dhana ya kuwa tusizibiane riziki. Najua kuna watu watakuja katika uzi huu na mtazamo huo. Lakini kwa mfano nilioutoa wa huyo muuza mihogo, angeweza kabisa kuweka biashara yake upande wa pili bila kubughudhi taratibu na usalama wa wengine, hili ndiyo lilinitatiza. Hawa watu hawaoni tofauti ya shambani na mijini.

Mji huu wa Dar baada ya miaka hii yote, kuna watu wengi sana wamestaarabika na wangependa kuishi katika mazingira ya kistaarabu na yote haya yanawezekana bila kuzuia mtu yoyote kutoka sehemu yoyote kuishi na kufanya biashara zake kwa kufuata taratibu.

Tatizo kubwa ninaloliona ni kuwa wengi wa watu wanaotoka vijijini wanakuja mijini na mitazamo ile ile ya huko walikotoka na wanalazimisha wengine wasalimu amri kwao. Na watu hawa hata wakae Dar miaka 20 hawezi kubadilika maana wakuja wapya wanaendeleza hizi taratibu na hivyo kushinikiza muendelezo wa fikra mbaya.

Nimeleta mada hii huku nikiheshimu harakati za kila mtu za kujitafutia riziki na pia napenda sana mchanganyiko wa mji wa Dar es Salaam ambapo hatuulizani makabila wala tulipotoka ila inahitaji nguvu ya ziada kuleta ustaarabu mjini hapa.

Hawa watu inabidi wakifika Chalinze, washushwe, wakalishwe kama wiki hivi pale wafundishwe taratibu za kuishi mijini zilivyo. Bila kufanya hivyo, huu mji hautabadilika kamwe nawaambia.
Mijitu ya bara haina ustaarabu
 
Nilichelewa kuja Dar ila sio mbaya sahivi vichochoro na mishe mishe nazijua. Mgeni uko Posta na Oysterbay uko.
 
Dah!Hata Paris ukienda haupewi semina elekezi ya kuishi aisee!DSM watu wengi wamevurugwa na hali ngumu ya maisha.

Muwe mnajipa hata likizo ya lazima mje huku vijijini kwetu mpumzike miezi miwili.Zawadi mtakazotuletea ni mikate tu.

Mnapoondoka tutawafungashia unga,mchele,maharage na hata kuku wazimawazima.Maana mmezoea utapeli na unyang'anyi.😂😂😂😂
Paris hawakupi semina elekezi kwa sababu wanajua ustaarabu wao na kwa kiasi kikubwa wageni wengi wanaenda huko na kuuheshimu.
 
Kuna Mkuu WA wilaya anaitwa Herri James naye anashiriki kuwakingia kifua Hawa watu
 
Kwani ni lazima watu wengi waishi Dar kwa shida??? Baadhi mrudi huku mikoani tufanye pamoja ujasiamali pamoja muone tunavyolipia Kodi ya flemu au mabatini na getto Wala hatufikirii kupanga bidhaa barabarani.
 
Back
Top Bottom