Wanaokula mihogo mibichi kupooza

Baba_Enock

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
7,076
Reaction score
2,457
Nimeonelea ni vyema ku-share hii habari na Wana-Jamii:

“Wakazi wa Dar es Salaam siku hizi naona wako katika hatari kubwa zaidi kwa sababu utakutana na akina mama wengi na mabeseni yao ya mihogo mibichi kichwani wakiwauzia watu kwa ajili ya kutafuna tu, ni hatari mno,” alisema Lweno

Source :HabariLeo | Wanaokula mihogo mibichi kupooza
 
Toka lini watanzania wakaheshimu tafiti za wanasayansi wao?
Toka lini watafiti wa kitanzania wakatoa elimu? Sasa huyu anatishia tu "ni hatari mno"! Mimi mwanakijiji wa mpandangindo nitaelewa nini? na machapisho yao ni kwenye magazeti yanayosomwa mijini tu! Huku shamba tunashindia kutafuna mihogo mibichi-"Hiyo ndiyo imetukuza"
 
Toka lini watanzania wakaheshimu tafiti za wanasayansi wao?

Mkuu lakini tafiti zingine huwezi kuzikubali. Kuna sehemu hapa nchini watu wamekula mihogo miaka inde irudi na ni jamii ambazo hazisumbuliwi na kupooza.
 
Mkuu lakini tafiti zingine huwezi kuzikubali. Kuna sehemu hapa nchini watu wamekula mihogo miaka inde irudi na ni jamii ambazo hazisumbuliwi na kupooza.

Inaonekana watu mnabisha kitu ambacho hamjakisoma na kukielewa vema. Mihogo inayosemwa kwamba ina madhara ni yenye ladha ya uchugu. Kwa wanaoifahamu vizuri mihogo huwa ipo yanye ladha tamu na yenye ladha ya uchungu. Na kuna mingine inakuwa na ladha ya kati siyo mitamu wala michungu.

Kitu ambacho nimeona huyo mtaalamu amekisema kwa ujumla ni kile cha kuamini kwamba mihogo yote inayouzwa Jijini DSM ina ladha ya uchungu. Kwenye habari iliyoko kwenye gazeti la habari leo Mtaalamu huyo amebainisha kwamba adhari zilizobainika Mtwara zilitokana na watu kula mihogo wakati wa njaa; sasa ni wazi kwamba nyakati za njaa huwezi kuna na fursa ya kuchagua mhogo mtamu au mchungu unachojali zaidi ni kupata shibe.

Mimi nakumbaka wakati tukikua ulikuwa ukila mihogo michungu mibichi miwili hivi (wakati wa kuchunga ng'ombe) ulikuwa unalegea au kulewa vile. Ni wazi hiyo ni dalili ya hiyo sumu kuwa ilikuwa inatuathiri.

Naafiki matokeo ya utafiti.
 
Ndugu zanguni ni kweli mihogo inaleata kupooza kwa viungo na hiii inatokana na sumu ya cyanide.
Kwa wale wanaokaa Mtwara naamini wameshaona hii na mara nyingi inatokea wakati wa njaa kwani mihogo mibichi inaandaliwa haraka bila na muda wa kutosha wa kuiosha na kupunguza sumu hiyo.
Nikijaaliwa nitawaletea picha ingawa ningependa nizifiche sura kwa ajili ya maadili.
Angalieni google cyanide poisonong in cassava au Konso disease
 
Na pia kuna uwezekano mkubwa tu wa kupata minyoo, japo athari hii ni ndogo ukilinganisha na hiyo cynide poisoning.
 
Hehehehehe, kama ni kweli basi 'kwishnei'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…